Mabingwa wa
mbio za Balimi Boat Race 2016 wakishangilia mara baada ya kushinda mbio za
kupiga makasia wakitumia dakika 34. Mashindano mbio za Makasia ni mara ya 16 yakidhaminiwa
na TBL kupitia bia ya Balimi Extra Lager,ambayo yalishirikisha vikundi 15 vya
mkoa wa kimechezo wa Ukerewe
Na
Mwandishi wetu,UKEREWE
VIKUNDI vya Wazee wa
Mamba (Wanauame)na Hapa Kati tu ( Wanawake),vya mkoa wa Michezo wa
Ukerewe, vimevunja rekodi ya mashindano ya mbio za Mitumbwi za Balimi Boat Race
2016 na kutwaa ubingwa na kujinyakulia vikombe medali za dhahabu na fedha
taslimu sh.2.2.
Mashindano hayo
yalifanyika juzi kwenye ufukwe wa Monarch hoteli wilayani Ukerewe, ambapo mgeni
rasmi Mkuu wa wilaya hiyo, Josephat Mkirikiti alikabidhi zawadi kwa washindi wa
mivhuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia ya
Balimi Extra Lager.
Bingwa wa
mashindano hayo kwa upande wa wanaume, kikundi cha Wazee wa Mamba kilitumia
dakika 31 kuweza kutwaa ubingwa huo na kukabidhiwa kombe,medali za dhahabu na
fedha taslimu, sh.1.2 ,huku Kikundi cha Hapa Kazi tu kwa wanawake,kiling’ara
kwa kushika nafasi ya kwanza, kikitumia dakika 39 na kukabidhiwa fedha taslimu
sh. 1,000,000,medali za dhahabu na kombe.
Nafasi ya pili kwa wapiga makasia
hao kwa wanaume ilikwenda kwa kikundi cha Kama Ipo Ipo tu kwa kutumia dakika 34
na kujinyakulia kitita cha sh.1,000,000, kikundi cha Ya Mtoto kilinyakua
nafasi ya tatu baada ya kutumia dakika 35 na kulamb sh.800,000 na nafasi
ya nne ilinyakuliwa na kikundi cha Tuliochelewa ambacho kiliondoka na
sh.600,000.
Vikundi vya Usipoteze muda, Nani
Kaona,Maisha ni kutafuta ,Mbeya City, Hapa Kazi tu na Ole wenu,vilivyoshika
nafasi ya tano hadi ya kumi,kila kimoja kilipata kifuta jasho cha sh.250,000.
Kwa upande wa wanawake,nafasi ya
pili ilikwenda kwa kikundi Kaza Roho,ambacho kilitumia dakika 41 na kikapata
sh.800,000, kikundi cha tatu cha Kazi na Malengo, kilitumiaz dakika 43 na
kubeba sh.600,000 na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Upendo na
kuzawadiwa sh.400,000.
Hata hivyo katika mashindano hayo
kikundi cha nahodha Yasinta kutoka Kirumba mtumbwi wazo ulipinduka na kuzama
lakini baada ya kuokolewa walibadili mtumbwi na kuendelea mashindano na
ukashika nafasi ya tisa.
Vikundi vitatu vy tabia Njema,
Mtafuta cha Uvunguni na Eberneza vilivyoshika nafasi ya tano hadi ya saba
walifutwa jasho kwa sh.200,000 kila kimoja, hata hivyo vikundi vitatu
viliondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kubainika vilishiri mashindano
kama hayo kwenye mikoa ya Mara na Mwanza, kimoja kikikishika nafasi ya kwanza
na kingine nafasi ya pili.
Akizungumza wakati akikabidhi
zawadi, Mkuu wa Wilaya, Mkirikiti, alisema kampuni ya TBL isichoke kupeleka
mashindano kama hayo wilayani humo kwa sababu wananchi wake wanapenda michezo
na burudani.
“TBL niwapongeze mnafanya vizuri
katika eneo la kodi,mmekuwa marafiki wa Uerewe sababu mmetufanya tuwe sehemu ya
maisha yenu.Changamoto yenu mtuangalie katika sekta za afya na elimu
(madawati).Mtusaidie hili la madawati na tupo tayari kuondoa vikwazo
vinavyowakwaza ili tuondokane na kero ya madawati,”alisema Mkirikiti.
Pia, aliipongeza kampuni hiyo kwa
kuwaondoa washiriki (mamluki) waliokwisha shiriki mashindano hayo mikoa
mingine,ambo walikuja kuchukua nafasi zizizo za kwao na katika eneo lisilo la
kwao.
Aidha, Meneja Mauzo wa TBL Kanda ya
Ziwa, Godwin Zacharia,alisema lengo la TBL kwa miaka 16 ya mashindano ya
Balimi, ni kukuza utamaduni na michezo ukiwemo wa kupiga makasia .
Alisema, kutokana na kukubaliwa na
jamii ya Kanda ya Ziwa,wataendelea kuyaboresha kwa kuongeza zawadi na washiri
kila mwaka kwa sababu bado wana kiu na kuahidi kushughulikia changamoto ya
washiriki bandia .
Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha
Mitumbwi Taifa-Tanzania Canoe Assocition,(TCA) Richard Mgabo alisema kuwa,
akiwa mwasisi wa mashindano ya makasia,anafarijika kuona mchezo huo ambao
haukuwepo nchini, ukipata mashabiki na kuzidi kupendwa na wananchi wa kada
mbalimbali na kuishukuru TBL kwa udhamini wao tangu yaanzishwe.