Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Sunday, January 29, 2012

ROGATH:EXTRA BONGO HAKUNA MWENYE NJAA,TUKO EXTRA BONGO KWA MAPENZI YA DHATI KUTOKA MOYONI YA KULETA MABADILIKO YA MZIKI WA DANSI NCHINI NA DUNIANI.

KIONGOZI wa Bendi ya Extra Bongo, Rogath Hega Katapila amekanusha usemi wa Mkurugenzi wa ASET-Twanga Pepeta, Asha Baraka kuwa hivi karibuni anatangaza dau ambalo anaamini atawarudisha wanamuziki wake walioondoka Twanga na kuhamia Bendi zingine haswa walio Extra Bongo.
Rogath amesema kuhama kwao kutoka Twanga si kwa pesa ba li ni mapenzi kutoka moyoni ya kuleta mabadiliko ya Muziki wa Dansi Nchini ndio uliowatoa Twanga,hawana mpango wa na wala hawategemei siku moja kurudi Twanga.
Amesema Kiongozi Rogath, Extra Bongo hakuna njaa hivyo ndoto zinazomsumbua atafute njia mbadala wa kuinusuru Bendi yake ya Twanga na si kufikiria wanamuziki kutoka Extra Bongo,.
Rogath amesema na swala la kuwataja taja majukwaani hawataki na kama ameshindwa mziki akagombea ujumbe wa mtaa tutambue kama kaingia rasmi kwenye siasa.

CHIEF KIUMBE AMPA BIG UP CKOCKY

Mkurugenzi wa Respect,Chief Kiumbe (kulia) akiwa na Mkurugrnzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky meeda Sinza jijini Dar es Salaam

MFADHILI Mkuu na Mpenzi namba moja wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo,Chief Kiumbe amekubali kwa kinywa chake kuwa Mkurugenzi Wa Extra Bongo alichokuwa anataka kukitengeneza sasa kinaonekana.
Chief ameyasema hayo baada ya kujionea mwenyewe jinsi Bendi hiyo ilivyo sasa kuwa ni moto wa kuotea mbali na hakuna mfano na wala hakuna mpinzani tena.
Chief baada ya kujionea sasa ameahidi kuisaidia zaidi Bendi hiyo kwa kila hali na mali na kwa kuanza ameahidi kununua vyombo vipya na vya kisasa ili mabadiliko yaliyopo Extra Bongo yaende sambamba na vyombo vipya.
Alisema Chief,sioni wapi kwa sasa kunatatizo kwani naona kila idara imekaa safi kuanzia wapiga vyombo,waimbaji mpaka wachezaji ni safi sana hapa ni kuboresha kwa kuongeza vyombo vipya na vya kisasa tu alimaliza Chief Kiumbe.

ATHANAS MOTANABE AAHIDI MAKUBWA EXTRA BONGO

Mwimbaji wa Bendi ya Extra Bongo, Athanas Michael (Motanabe) akiimba wimbo wa rumba wa Neema

MWIMBAJI mwanzilishi na kipenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Athanas Motanabe atamba kufanya makubwa katika Bendi ya Muziki wa Dansi kwa mwaka 2012.
Akizungumza na mtandao huu, Athanas amesema wakiwa katika harakati za kurekodi video kukamilisha Albam ya Bendi yake lakini pia yuko msituni kwa sasa kutunga vibao vipya ambavyo anaamini vitawafanya wapenzi na mashabiki kuamini kuwa sasa Extra Bongo hawapimiki wala kufananishwa na Bendi yeyote Tanzania na Duniani.
Athanas kwa sasa anatamba na kibao cha zuku cha Neema ambacho tayari amesha maliza kurekodi na muda si mrefu wapenzi na mashabimki wakae mkao wa kukisuhudia kwenye Luninga pamoja na zingine nyingi

MISS KISWAHILI ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA

MISS Kiswahili Tanzania, Rehema Fabian amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa aina ya pekee ambapo amejumuika na Watoto Yatima wa Kituo cha Kuwama kilichopo Mwenge Jijini Dar es Salaam
Akizungumza na mtandao huu Rehema amesema nimefanya hivi ili kuikumbusha jamii haswa Warembo wenzangu na Mastaa kwa ujumla kuwa kuna wenzetu ambao wanahitaji faraja ya pekee na haswa tunapowashirikisha furaha zetu kama hivi
Watu wengi wanapokuwa na furaha binafsi hujumuika na ndugu ama marafiki na kufanya makamuzi ya kufa Mtu lakini pia tunapowakumbuka hawa ambao hawamjui Mama wala Baba ni jambo jema mbele ya jamii na kwa Mwenyezi Mungu pia
Rehema Fabiani ni Mrembo anayeshikilia taji la Miss Kiswahili Tanzania kwa sasa,wito wake kwa jamii ya watanzania na haswa kwa watu wenye uwezo ama nafasi tuwakumbuke watoto Yatima amesema Rehema
Miss Kiswahili Tanzania, Rehema Fabian akimlisha Mtoto wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa

Miss Kiswahili Tanzania akiwa na baadhi ya Watoto Yatima wa Kituo cha kulelea cha Kuama cha Mwenge Dar es Salam

SUPER NYAMWELA ATAMBULISHA NYIMBO YAKE MPYA.




KIONGOZI wa wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo,Hassan Mussa(Super Nyamwela) ametambulisha nyimbo yake mpya ya Bakutuka katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Akiimba sambamba na waimbaji wengine wakiwemo,Athanas Motanabe, Suleiman Ramadhan(Suzuki), Rama Pentagon,Frank Almas(Kabatano),Redo Mopasa (Mauzo), na Emanuel Michael (Bob Kissa) ambapo walimba sambamba na shoo kali ambayo iliwafanya mashabiki waliohudhulia onyesho hilo kuachia viti na kusimama.
Akizungumza na mtandao huu, Super Nyamwela amesema ameamua kuimba ili kuwapa mashabiki wake kachumbali na kuwazihilishi kuwa si kucheza tu bali hata kuimba pia anaweza.
Wimbo wa Nyamwela ndio unaofunga albam mpya ya Extra Bongo ambayo kwa sasa wako Studio wakiandaa Video yake ambapo tayari nyimbo mblili zimeshakamilika na tayari zimeashaanza kupigwa kwenye vituo vya Televisheni lakini bado hawajaipatia jina albam hiyo.
Nyamwela ambaye amedhamilia kuleta mapinduzi ya mziki wa dansi nchini na Dunia nzima kupitia Bendi ya Extra Bongo kwa sasa anaandaa shoo kali ya aina yake ambayo anasema itakuwa historia kwa watanzania na Dunia nzima.

EXTRA BONGO SASA WANATISHAAAAAA.........

Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza wakati wa onyesho la Bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Meeda
Wakicheza kwa staili ya pekee

Haya sasa

Twende sasa.........

Mh..........
Hapo..........

Haya sasa..... Twende sasa......



Hapo.......

Suzuki sasa moto x3

Bob Kissa akilalamika na nyimbo ya Mama Shu..

Athanas akilalamika na nyimbo ya Neema...

Aha........



Kiduku

Joshua Bass akifanya vitu vyake

Rapa Fagason akirap sambamba na wacheza shoMh.....

Thursday, January 19, 2012

SUZUKI NDANI YA EXTRA BONGO- ANASEMA SASA NI MOTO X3 NA LEO NI NDANI YA MZALENDO PUB.

Mwimbaji wa Bendi ya Extra Bongo, Selemani Ramadhani (Suzuki sauti ya malaika) akiimba wakati onyesho la bendi hiyo linaloendelea mzalendo Pub Kijitonyama Dar es Salaam sasa hivi.

Na Michael Machellah
Ni mwanamuziki Nguli wa Extra Bongo aliyevuma sana enzi fulani za Bendi hiyo haswa katika Albam ya Mjini mipango baade aliamua kupumzika na kujiunga na Bendi fulani Mji kasoro Bahari nazungumzia Morogoro
Selemani Ramadhani(Suzuki) ni mwanamuziki tishio haswa anapokaa stajini,Leo live yupo katika Bendi yake ya awali ya Extra Bongo bendi yake aliyokuwa akiimbia enzi hizo anasema sasa amerudi nyumbani kujenga nyumbani kwake kule alikoanzisha kila kitu
Suzuku anasema wapenzi na mashabiki wake njooni Extra Bongo njooni mzalendo mpate mambo mazuri kutoka kwake na kwa Bendi nzima ya Extra BONGO.

H-BABA AKAMILISJA SINA RAHA NA BANZA STONE

Na www.sufianimafoto.blogspot.com

MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Ramadhan ‘H-Baba’ amekamilisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Sina Raha, akimshirikisha gwiji wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja, ‘Banza Stone’ Mwalimu wa Walimu.
Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto, H-Baba, alisema kuwa kibao hicho ni miongoni mwa nyimbo zake 10 zitakazokamilisha albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Shika hapa acha Hapa’ inayotarajia kuingia sokoni mwezi wa tatu mwaka huu.
Aidha alisema kuwa wimbo ambao amemshirikisha Banza Stone, amerokodia katika Studio ya Allan Mapigo, ambapo tayari amekamilisha maandalizi ya kurekodi video ya wimbo huo mwishoni mwa wiki hii.
H-Baba alisema kuwa katika wimbo huo mashabiki wake watarajie kupata vitu tofauti ikiwa ni pamoja na staili mpya na midundo iliyo ‘shiba’ na sauti murua ya Banza Stone, aliyeonyesha uwezo wake katika wimbo huo.
Alizitaja studio alizorekodia nyimbo zake zitakazokamilisha albam hiyo kuwa ni pamoja na KGC Studio, Maneke Studio na Allan Mapigo, zote za jijini Dar es Saam.
Pia alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwamo katika albam hiyo kuwa ni pamoja na, Nipe Kidogo, Shika Kichwa, Kinacho Niumiza, Zaidi yako Wewe na Nimpende Nani.

Wednesday, January 18, 2012

KIFAA HIKI UNAWEZA KUKIFANANISHA NA NANI-NIPE JIBU KUPITIA EMAIL YANGU




KIFAA HIKI UNAWEZA KUKIFANANISHA NA NANI-NIPE JIBU KUPITIA EMAIL YANGU
Ni Dereva wa Bajaji maeneo ya Wilaya ya Kinondoni haswa hupenda kupaki maeneo ya Kijitonyama na Sinza maeneo ya Kona Bar wakati mwingine.
Niligongana nae nikiwa katika mishe mishe zangu za kuwahi hapa na pale katika kupata habari,nikasimamisha Bajaj yake ili niwahi ninakokwenda hswa nikwambie nilikuwa naelekea pale Mzalendo Pub ambako Bendi ya Extra Bongo walikuwa wanatumbuiza pale siku hiyo,baada ya kusimamama kifaa hicho ukweli hakili yangu ilinituma kuwa ni Msanii marufu Nchini ambaye kwae ananifahamu nikahisi kasimama kwasababu ananifahamu na si dEREVA Bajaj ambaye anatafuta abiria.
Nilitoa hai nikijua ni Msanii ambaye tunafahamiana katika mazingira ambayo unayafahamu ya watu wanaofahamiana,ukweli mshikaji kulingana na tabu anazozipata kwa watu wengi aliniitikia kwa furaha lakini baadae alichana na kiambia najua umenifananisha na msanii fulani akamtaja.
Sio mimi na si wewe tu watu waengi wananifananisha,huyo mtu simjui na sijui kabila gani lakini baada ya watu kunigasi hivi karibuni ndio nimemuona kupitia TV ni kweli tunafanana labda sijui wazazi wetu alisema mshikaji,ninahamu sana ya kukutana nae huyu jama tufahamiane alimaliza......
Embu umiza kichwa kisha nitumie email au kupitia coments.

MADAU RACHEL SINBARD ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA SHANGWE NA VIGELEGELE

Rachel akiwa na keki mkononi akiwa tayari kuwalisha marafiki zake wakati wa kuadhimisha siku yae ya kuzaliwa
Rachel akikata keki

Rachel na marafiki zake chumbani kwake wakati wa sherehe yake

Keki zilizokuwepo wakati wa hafla ya kukumbuka siku yake ya kuzaliwa mdau rachel Sinbard hafla fupi iliyofanyika chumbani kwake hapo jana.Keki ya Kushoto ililetwa na Rafiki zake anaoishi nao Chumbani(Roommates) na keki ya Kulia ililetwa na Shemeji yake Aitwaye Angaza Nkurlu

Tuesday, January 17, 2012

RATIBA YA EXTRA BONGO WIKI HII

Mwimbaji wa Bendi ya Extra Bongo, Athanas Motanabe akiimba wakati wa onyesho la Bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza Jijini Dar es Salaam


RATIBA YA EXTRABONGO

BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo wiki hii wataanza na siku ya Alhamisi ambapo watatumbuiza kwenye Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama jijini Dar es Salam,Ijumaa ni Boko CCM Calfon Pub ,Jumamosi ni kwenye Ukumbi wa nyumbani Meeda Sinza Jijini Dar es Salaam na Jumapili ni Dar live Mbagala jijini Dar es Salam

Mpiga tumba wa Bendi ya Extra Bongo, Salum Issa Mkanje (Chakuku Tumba) akiwajibika wakati wa onyesho hilo


Chakuku.............. Mwimbaji wa Bendi ya Extra Bongo, Ramadhani Mhoza (Rama Pentagon) akicheza sambamba na wacheza shoo wa Bendi hiyo Wakicheza Wakicheza Wakiwajibika Mcheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo, Danger Boy akicheza sambamba na shabiki wa bendi hiyo Mpiga Bass wa Bendi ya Extra Bongo, Hoseah Mgoachi akilichakaza bass mbele ya shabiki Shabiki wa Bendi ya Extra Bongo,Maarufu kwa jina la Babas Meneja wa Respect akimtunza Mkurugenzi wa Extra Bongo , Ally Chocky Chocky akirap sambamba na wacheza shoo wake Wacheza shoo wa Extra Bongo wakiwajibika jukwaani

Saturday, January 14, 2012

EXTRA BONGO SASA TISHIO TANZANIA

Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza Jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho lao la kila wiki
Wakicheza

Na Michael Macellah

BENDI ya Muziki wa Dance inayotikisa jiji la Dar es Salam na Tanzania nzima,Extra Bongo Next Level baada ya kukonga nyoyo za wapenzi na mashabiki katika kipindi cha sherehe za X-Mass na Mwaka mpya sasa wanaelekea kujikita na kurekodi nyimbo zao zilizosalia ili kukamilisha Albamu yao ambayo mpaka sasa hawajaipatia jina.


Akizungumza na mtandao huu,Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Chocky ameanza kwa kuwashukuru wapenzi na mashabiki kwanza kwa kuiunga mkono Bendi ya Extra Bongo katika kipindi chote cha siku Kuu na kuwaomba sasa wakae mkao wa kusubili mambo mapya na mazuri ya bendi hiyo ambayo watawatambulisha hivi punde mara tu ya kumaliza kurekodi.


Amesema Chocky 'tunaingia jikoni kupika vinavyopikika tunaamini tunachowaandalia mtakipenda na mtakifurahia hivyo kaeni mkao wa burudani muda si mrefu tutawafahamisha'.


Chocky amesema Bendi katika kuhakikisha inaweka mambo sawa kila mahali katika safu mbalimbali ndani ya Bendi, Bendi imeongeza waimbaji wawili,Kaba tano na Redo walikuwa TOT na wa tatu ni rapa ambaye alipumzika muda fulani lakini sasa amerejea kazini.


Katika safu ya wapiga vyombo pia ameongeza mpiga bass,tumba,drum na soro na katika safu ya wacheza shoo imeongeza watatu wa kike akiwemo Janeth Tingisha aliyekuwa Diamond Sound na mmoja wa kiume. Wacheza shoo na waimbaji wakicheza Waimbaji na wacheza shoo wakicheza kwa pamoja


UTAMBULISHO WA CHARLES BABA NA 33 MASHUJAA MUSICA BAND, 33 ANG"ARA ZAIDI

33 akiimba wakati wa utambulisho wake na Charlez Baba katika Bendi ya Mashujaa Musica Bendi kwenye Ukumbi wa Busness Complex Victoria jijini Dar es Salaam
Charlez Baba akiimba wakati wa utambulisho wake

Harid Chokoraha akimtunza Charlez Baba wakati wa utambulisho wake

Dogo tulia kula Bata mashujaa

Kalala Junia akimtunza Charlez Baba

Jose Mala akimtunza Charlez Baba

Umati wa watu wakishuhudia utambulisho wa Charlez Baba ba 33

Meneja wa Mapacha watatu, Dakoda akiwataka wanamuziki hao kukumbushia enzi zao mara baada ya kukutana kiwanja kimoja

Mapacha watatu na Fagasoni na Carles Baba wakikumbishia enzi zao za Bendi fulani huko nyuma wakati wa utambulisho wa Charlez Baba na 33

Harid Chokoraha akiimba sambamba na Charlez Baba


Kalala Junia akiimba sambamba na Charlez Baba

Chaelez Baba akiimba sambamba na Jose Mara

Saullo Fagason akirap wakati Jose,Chokoraha,Charlez na Kalala wakicheza

Saullo Fagason akirap wakati Chokoraha akicheza kwa staili ya peke yake

Fagasoni akisema jambo mara baada ya kumaliza kuimba wimbo huo