Friday, August 31, 2012
Wakali kutoka WATANASHATI ambao leo watakuwa wakifanya mavituziiiiiiiii na EXTRA BONGO ndani ya UKUMBI wa NEW WHITE HOUSE -Kimara -Korogwe.Kiingilio cha ubwete tu ni 5000/=
Thursday, August 30, 2012
RATIBA YA WIKI HII
IJUMAA ni ndani ya ukumbi wa NEW WHITE HOUSE-Kimara Korogwe WAKISHIRIKIANA NA KUNDI ZIMA LA WAKALI WA BONGO FLEVA KUTOKA WATANASHATI[mzee wa mauzo SHARO MILIONEA,PNC,DOGO JANJA] na burudani zitaanza saa 3 Usiku na KIINGILIO ni 5000/=
JUMAMOSI ni kama kawaida katika Ukumbi wa MEEDA Sinza.
JUMAPILI mwisho wa wikiend ni katika Ukumbi wa nyumbani NEW WHITE HOUSE Kimara Korogwe na hii itakuwa FAMILY BONANZA,Muda ni kuanzia saa kumi jioni
NYOTE MNAKARIBISHWA
a.k.a WAZEE WA SCANDINAVIA-EXTRA BONGO na KUNDI ZIMA LA WATANASHATI-Ijumaa hii 31/08/2012
Burudani ni moja 2 siku ya Ijumaa na itakuwa ndani ya ukumbi wa NEW WHITE HOUSE-Kimara Korongwe- Ambapo makumbi mawili ya vijana watoa burudani za ukweli EXTRA BONGO[Next Level]chini yake Director ALLY CHOKI na WATANASHATI GROUP chini ya vijana wakali wa BONGO FLEVA mkali PNC,DOGO JANJA na mkali wa mauzo SHARO MILIONEA watatoa burudani ya kufa m2 siku hiyo na KIINGILIO NI 5000/= na SHOW itaanza saa 3 USIKU
Tuesday, August 28, 2012
ACHANA NA UZUSHI-Hiki ndio kikosi kamili cha wanamuziki wa Extra Bongo kilichorejea kutoka ulaya wiki mbili zilizopita.
Wednesday, August 22, 2012
EXTRA BONGO WAJA NA MOTO MKALI MKUTOKA ULAYA,WAITEKA KIMARA SIKU KUU YA EID,MEEDA PAFURIKA EID PILI
Wacheza shoo wa kike wa Band ya Extra Bongo wakicheza wakati wa onyesho maalum la siku Kuu ya Eid pili katika Ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam
Mwimbaji na Kiongozi wa wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo, Super Nyamwela akiima wakati wa onyesho hilo
Mpiga Bass, Hoseah Mgoachi akilichalaza gitaa sambamba na wacheza shoo wakati wa onyesho hilo
Wacheza shoo wa kike wa Band ya Extra Bongo wakicheza wakati wa onyesho maalum la siku Kuu ya Eid pili katika Ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam
Friday, August 17, 2012
EXTRA BONGO WAFUTURU NA WATOTO YATIMA
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo akifuturu pamoja na Watoto yatima wa kituo cha kulelea watoto hao cha New Life kilichopo Kigogo jijini Dar es Slaam
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki wakiwa na Mkurugenzi wa kituo cha Kulele Watoto Yatima cha New Life
Na Michael Machellah
BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo leo imefuturu pamoja
na Kituo cha Watoto Yatima cha Home New Life kilichopo Kigogo jijini Dar es
Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Bendi ya
Extra Bongo, Ally Chocky amesema wamefanya hivyo ili kuonyesha upendo kwa
watoto hao ambao pengine kwa kipindi kama hiki wangekuwa na Wazazi wao lakini
kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu wako katika mazingira hayo na si kwa ridhaa yao.
Alisema Chocky wao kama sehemu ya jamii inayowazunguka
watoto hao hawanabudi kufanya hivyo angalau hata Watoto hao nao wajitambue kuwa
kana jamii inawazunguka na inatambua uwepo wao.
Chocky alisema kwa mfano huo anawaomba hata Bendi zingine
waige mfano huo na si bendi tu bali hata watu binafsi kwani Watoto hao ni wetu
sote hatuna budi kuwafariji na kufurahi pamoja nao tupatapo nafasi.
Bendi ya Exta Bongo sasa iko kwenye mazoezi makali
ikijiandaa na maonyesho ya Idd mosi na Idd pili ambapo Idd mosi wanatarajia
kufanya onyesho katika Ukumbi wao wa New White Kimara na Idd pili watakuwa
katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam.
Watoto Yatima wa kituo cha New Life wakifuturu pamoja na wanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo
Mwimbaji wa Bendi ya Extra Bongo, Rama Pentagon akigawa maadazi kwa watoto wakati wa futari hiyo
Wednesday, August 8, 2012
ALLY CHOCKY AKIKATA MITAA YA ULAYA
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo akikata mitaa na baadhi ya wanamuziki wakewakati wa ziara ya Bendi yake Barani Ulaya
Baadhi ya Wanamuziki wa Extra Bongo wakiwa katika picha ya pamoja na mashabiki wa muziki wa Dansi Barani Ulaya
Tuesday, August 7, 2012
EXTRA BONGO WAREJEA NCHINI BAADA YA MAKAMUZI YA TAKRIBANI MWEZI ULAYA
TIMU ya wanamuziki 15 waliokuwa wamesafirio kwenda Ulaya kwenye Tamasha la First Afrika hatimaye wamerejea Nchini baada ya kufanya makamuzi ya takribani mwezi mmoja.Akizun gumza na waandishi wa habari,Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Chocky amesema ziara yao ilikuwa ni kvutia walipokelewa vizuri na katika mamonyesho yao yote yamevutiwa sana na watu haswa waishio Barani Ulaya na Waafrika wenzetu
Bendi ya Extra Bongo sasa itaendelea na mazoezi kama kawaida wakijiandaa na sikukuu ya Idd ambapo wanatarajia Idd mosi kufanya onyesho kwenye Ukumbi wao wa White House Kimara na Idd pili wanatarajia kufanya onyesho katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam
Friday, August 3, 2012
Thursday, August 2, 2012
EXTRA BONGO WAENDELEZA MAKAMUZI KATIKA JIJIJ LA TEMPERE FINLAND
Wacheza shoo wa kike wa Bendi ya Extra Bongo wakiongozwa na kiongozi wa wacheza shoo wa kike, Otilia Boniphace wakicheza wakati wa onyesso lao maalum jijini Tempere Finland
Kiongozi wa wawacheza shoo, Super Nyamwela akicheza wakati wa onyesho hilo
Mpiga Bass, Hoseah Mgoachi akilichaka Gitaa wakati wa onyesho hilo
Danger Boy akicheza wakati wa onyesho hilo
Waimbaji wakicheza wakatiti wa onyesho hilo,kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bendi hiyo, Ally Chocky, Bob Kissa na Athanas Motanabe