Baadhi ya
wachezaji wa Klabu ya Mpo Afrika wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuibuka
mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa,Mkoa
wa Temeke iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Mpo Afrika ilishinda
13-11 dhidi ya Klabu ya Sun City.
Katibu
Mkuu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga akimkabidhi zawadi ya fedha
taslimu shilingi 350,000/= bingwa wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles),
Sulemani Cato mara baada ya kumfunga Nahodha wa timu ya Taifa Charles Venance
4-2.Dar es Salam mwishoni mwa wiki
Mchezaji wa
timu ya Klabu ya Mpo Afrika na Nahodha wa timu ya Taifa, Charles Venance
akicheza wakati wa mechi ya fainali dhidi ya klabu ya Sun City wakati wa
mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Temeke iliyofanyika
mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi
Wetu.
TIMU ya Mpo Afrika ya Mkoa wa
kimichezo ya Temeke jijini Dar es Salaam imetwaa ubingwa wa mkoa baada ya kuifunga
timu ya Klabu ya Sun City 13-11, katika fainali za mashindano ya mchezo
wa Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika
ukumbi wa Klabu ya Bushnet Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam. Mpo afrika kwa ushindi huo ilizawadiwa Kikombe, fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Temeke katika fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika mwezi ujao Mkoani Morogoro.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na klabu ya Sun City na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/= na nafasi ya tatu katika mashindano hayo ilichukuliwa na Klabu ya Kurasini ambayo ilizawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/= na mshindi wa nne ni klabu ya Bushnet ambao ndio walikuwa wenyeji wa mashi ndano hayo.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Mchezaji waKlabu ya Bushnet, Sulemani Kato(Shetani) alifanikiwa kuchukua ubingwa kwa kumfunga Charles Venance 4-2 na kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa kimichezo wa Temeke katika fainali za kitaifa Mkoani Morogoro.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na mchezaji Charles Venance kutoka klabu ya Mpo Afrika ambapo alizawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/= na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mchezaji, Amos Boniphace ambaye alizawadiwa 150,000/= na nafasi ya nne ni Hassan Abdubakar.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake (Singles), Beatrice Charles alitwaa ubingwa kwa kumfunga Madina Idd 4-0 na hivyo kujinyakulia zawaadi ya fedha taslimu shilingi 250,000/= pamoja na tiketi ya kwakilisha mkoa wa Temeke katika fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Madina Idd ailichukua nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/= .Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Manka Mushi ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 100,000/= na nafasi ya nne ni Rebeka Magaigwa ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 50,000/=.
Akizungumza na wachezaji kutoka vilabu vyote, Katibu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga aliwaomba klabu iliyotwaa ubingwa na ambayo itawakilisha mkoa wa Temeke katika fainali za kitaifa mkoani Morogoro kujiandaa vyema kwani ushindani ni mkubwa huko wanakoelekea na pia wazingatie nidhamu kwani bila nidhamu inaweza kuwafanya wasifanye vizuri mbele ya safari.
Mwisho aliwshuikuru TBL, kupitia bia ya Saafari Lager kwa kuendelea kufadhili mashindano hayo ambapo aliwaomba wapenzi wa pool kunywa Safari Lager ili waendelee kuwa wafadhili wakuu wa mashindano ya Pool.
Mashindano ya Safari Pool Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni ulishirikisha vilabu tisa ambavyo ni Mpo Afrika, Sun City, Kurasini,Bashnet,BMK,Sifa Mtoni,MTN,Amazoni na SuperStar.
Wachezaji wa Klabu ya Mpo Afrika wakifuatilia mchezo kwa makini
Baadhi ya Wachezaji wa Sun City wakishangilia wakati wa mechi ya Afrika
Mwamuzi wa mechi ya fainali,Yamini akiwaamuru wachezaji kulagi
Baadhi ya wadau wakifuatilia mchezo
Mcheaji wa Sun City akicheza
Wachezaji na mashabiki wa Klabu ya Mpo Afriaka wakishangilia mara baada
ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa
ngazi ya Mkoa, Mkoa wa kimichezo wa Temeke
Katibu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga akimkabidhi zawadi bingwa
wa single wanawake,Beatrice Charles fedha taslimu shilingi 250,000/=
Katibu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga akimkabidhi mshindi wa pili
singles wanaume,Charles Venance fedha taslimu shilingi 200,000/=
Mpo Afrika wakishangilia wakati bingwa wa Singles wanaume,Sulemani Cato akichukua zawadi
Mpo wakishangilia
Nahodha wa timu ya Mpo,Charles Venance akikabidhiwa Kikombe
Wachezaji wa Mpo wakishangilia na Kikombe
Mkurugenzi wa Mpo Afrika akishangilia na Kikimbe mara baada ya timu yake
kutwaa ubingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa Ngazi
ya Mkoa, Mkoa wa Temeke kumalizika mwishoni mwa wiki
Mkurugenzi akishangilia kwa furaha
Mpo Afriaka wakishangilia na Kikombe |
0 maoni:
Post a Comment