Meneja
Mauzo na Usambazaji
wa Samsung Tanzaia , Sylvester Manyara (kushoto) akimkabidhi funguo
mshindi wa gari ya Pambika na Samsung
Mitsubishi Double Cabin, Juma Mussa Ramadhani katika promosheni ya
Pambika na Samsung iliyomalizika leo Mlimani City jijini Dar es
Salaam.Kulia ni msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha
Tanzania, Bakari Maggid.
Juma Mussa Ramadhani akifurahia mara baada ya kukabidhiwa funguo
Pambika
na Samsung yatangaza mshindi wa Mitsubishi Double Cabin
Promosheni ya msimu wa
sikukuu za mwisho wa mwaka ya Pambika na Samsung imefikia tamati Jumatatu baada
ya kumshuhudia mshindi wa droo kubwa ya mwisho Bw. Juma Musa Ramadhan (46)
ambae ni mfanyabiashara akiibuka mshindi wa jumla wa zawadi kubwa ya gari. Bw. Juma
Sasa ndie mmiliki mpya wa gari aina ya Mitsubishi Double Cabin iliyosheheni
zawadi kibao toka Samsung ikiwa pamoja na Kompyuta mpakato, Mashine ya kufulia
nguo, Jokofu, Galaxy Tab 10.1, jiko la kupashia chakula, Luninga ya LED 32’,
deki ya DVD na muziki wa nyumbani.
Akionyesha kutoamini
anachokisikia toka upande wa pili wa simu iliyompigia kumtambulisha kuwa mshindi
wa Pambika na Samsung, bw. Juma Musa alijawa na furaha yenye mshangao baada ya
kupokea simu iliyomtambulisha kuwa yeye ni mshindi wa zawadi ya gari. “Kusema
kweli sikuwa nashawishika kabisa kwamba nimeshinda gari jipya aina ya
Mitsubishi Double Cabin. Nimejikuta mwenye furaha kupitiliza, ni ngumu kukubali
ukweli kwamba nimeshinda gari, sikuwahi kufikiria kitu kama hiki! Nimefurahi
sana!,” alisema Bw. Juma mkazi wa Tabata Segerea jijini Dar es salaam.
Droo hiyo ya mwisho
iliyofanyika katika eneo la kibiashara la Mlimani City jijini Dar es salaam pia
ilishuhudia washindi wengine 15 wakijishindia zawadi mbalimbali toka Samsung
katika kufunga pazia la mwisho la promosheni hiyo ambapo tayari imeshawazawadia
jumla ya watu 90 toka kuanza kwake.
Pambika na Samsung ilikuwa
ni promosheni ya wiki 7 ambayo ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi Novemba ikiwa na
lengo kuu la kuwazawadia wateja wa Samsung wanaonunu bidhaa halisi za Samsung
na kuzisajili kwenye mfumo maalum wa dhamana. Ujumbe wa kampeni si tu
kuwazawadia wateja bali pia kutoa fursa na kuahamsisha Watanzania kuangalia
uhalisia na uhalali wa bidhaa wanayonunua kupitia maduka ya Samsung au mawakala
waliosajiliwa na Samsung.
Akizungumza mapema na
waandishi wa habari, Meneja mauzo na Usambazaji wa Samsung Tanzania, Bw
Sylvester Manyara alisema kwamba, “Promosheni hii imekuwa ni safari yenye
mafaniko kwa Samsung Tanzania toka kuanza kwake na tungependa kumshukuru kila
mmoja kwa kuwa sehemu ya mabadiliko na mafanikio. Promosheni hii imeonyesha
ongezeko la 30% la wateja wanaosajili bidhaa zao kwa hiari katika mfumo wetu maalum
wa dhamana ya ziada” alisema bw. Manyara.
“Kuonyesha mafanikio,
kampeni hii ni moja kati ya mipango ya muda mrefu ya Samsung katika kukabiliana
na tatizo la bidhaa feki nchini Tanzania na kuongeza uwelewa juu ya faida za
kununua bidhaa halisi. Ni matarajio yetu kwamba huu utamaduni wa kununua bidhaa
halisi utaendelea hata mara baada ya kumalizika kwa promosheni ya Pambika na
Samsung” aliongezea Bw. Manyara
Pambika na Samsung ilikuwa
ni moja ya promosheni kubwa iliyoendeshwa na Samsung Tanzania ambayo ilikuwa ni
kampeni ya kitaifa maalum kuwazawadia wateja 15 katika droo za kila wiki katika
kipindi cha wiki saba ikifuatiwa na droo kubwa ya kutoa zawadi kubwa ya gari
kwa mshindi wa jumla.
Meneja
Mauzo na Usambazaji
wa Samsung Tanzaia , Sylvester Manyara (kushoto)akimpongeza mshindi wa
gari, Juma Mussa Ramadhani mara baada ya kumkabidhi gari yake katika
promosheni ya Pambika na Samsung iliyomalizika leo Mlimani City jijini
Dar es Salaam.
Hivi ndivyo Juma Mussa Ramadhani alivyopatikana katika droo hiyo, Hapa akipigiwa simu
Msindi wa Gari, Juma Mussa Ramadhani (wa pili kulia) alipowasili
Mlimani City mara baada ya kupigiwa simu kuwa kashinda gari katika
promosheni ya Pambika na Saamsung.
Juma Mussa Ramadhani akisimulia ilivyokuwa mpaka ameshinda
Hongera sana
0 maoni:
Post a Comment