Na Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' Amin na kundi la Sanaa la Makhirikhiri wa bongo ni miongoni mwa burudani
zitakazosindikiza onyesho maalumu la 'Usiku wa Banza Stone' la bendi ya Extra Bongo 'Next Level' Wazee wa Kizigo kwa ajili ya
kumtambulisha mtunzi na mwimbaji wake Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anayerejea upya jukwanii Jumamosi hii
ndani ya Meeda Club Sinza jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika na tayari Banza ameanza mazoezi
makali ya kufua sauti yake tayari kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi waliokuwa wame-mis sauti na
tungo zake.
Kwa muda wa miezi mitatu Banza alikuwa yu mgonjwa hali iliyomsababishwa kushindwa kupanda jukwaani kabla ya mwishoni
Alisema, Amin na Makhirikhiri wa Bongo ni sehemu tu ya burudani zitakazopamba 'usiku wa Banza Stone' kwani kutakuwa na
vikundi vingine vya sanaa vitakavyonogesha onyesho ambapo mara baada ya onyesho hilo wataendelea kumtambulisha Banza
katika kumbi mbalimbali za burudani jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya ziara nyingine katika baadhi ya Mikoa.
RATIBA NA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA RAUNDI YA PILI, KAGERA SUGAR vs MBEYA CITY KUCHEZWA KAITABA STADIUM JUMAMOSI, YANGA VS ASHANTI UNITE TAIFA

Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Jumamosi kwa mechi tano katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam, Tanga wakati mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting inahamishiwa uwanja mwingine.
Ashanti United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union itacheza na Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar.
Jumapili (Januari 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Mgambo Shooting itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na Rhino Rangers zitaumana kwenye Uwanja wa Taifa.
Mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine inahamishiwa uwanja mwingine kwa vile huo bado nyasi zake ambazo zimepandwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili mechi hiyo.
Hivyo Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta uwanja mwingine unaokidhi viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Januari 29 mwaka huu.
Pia matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu kwa vile viwanja nane ambavyo tayari vimefungwa vifaa vya tiketi hizo. Vilevile tunakumbusha washabiki wa mpira wa miguu kuwa tiketi za elektroniki haziuzwi viwanjani.
SIMBA SC 2, KAGERA SUGAR 2 walipotoshana nguvu msimu uliopita na Simba
Wachezaji wakisalimiana.
Kikosi cha Mbeya City kilichopambana na Azam FC katika msimu wa kwanza
NO
|
TEAMS
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
PTS
|
1
|
Young Africans |
13
|
8
|
4
|
1
|
31
|
11
|
20
|
28
|
2
|
Azam FC |
13
|
7
|
6
|
0
|
23
|
10
|
13
|
27
|
3
|
Mbeya City |
13
|
7
|
6
|
0
|
20
|
11
|
9
|
27
|
4
|
Simba SC |
13
|
6
|
6
|
1
|
26
|
13
|
13
|
24
|
5
|
Kagera Sugar |
13
|
5
|
5
|
3
|
15
|
10
|
3
|
20
|
6
|
Mtibwa Sugar |
13
|
5
|
5
|
3
|
19
|
17
|
2
|
20
|
7
|
Ruvu Shootings |
13
|
4
|
5
|
4
|
15
|
15
|
0
|
17
|
8
|
Coastal Union |
13
|
3
|
7
|
3
|
10
|
7
|
3
|
16
|
9
|
JKT Ruvu |
13
|
5
|
0
|
8
|
10
|
16
|
-6
|
15
|
10
|
Rhino Rangers |
12
|
2
|
4
|
6
|
9
|
16
|
-7
|
10
|
11
|
JKT Oljoro |
13
|
2
|
4
|
7
|
9
|
19
|
-10
|
10
|
12
|
Ashanti United |
13
|
2
|
4
|
7
|
12
|
24
|
-12
|
10
|
13
|
Tanzania Prisons |
12
|
1
|
5
|
6
|
6
|
16
|
-10
|
8
|
14
|
Mgambo JKT |
13
|
1
|
3
|
9
|
3
|
23
|
-20
|
6
|
RATIBA
RAUNDI YA PILI
25 Januari 2014
Ashanti United vs Yanga
Azam FC vs Mtibwa Sugar
Coastal Union vs JKT Oljoro
Kagera Sugar vs Mbeya City
Tanzania Prisons vs Ruvu Shootings
JKT Ruvu vs Mgambo JKT
Jumapili, 26 Januari 2014
JKT Ruvu vs Mgambo JKT
Simba vs Rhino Rangers
Tanzania Prisons vs Ruvu Shootings [Imeahirishwa, Sababu ya Uwanja]
PSPF YATOA PONGEZI KWA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA WIZARA YA FEDHA
MFUKO WA PENSHENI WA (PSPF)
SALAMU ZA PONGEZI
Waziri wa Fedha Mhe.
Saada Mkuya Salum (MB)
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mh. Adam K. Malima.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa
kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.
Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa
Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima.
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wote wamepokea kwa furaha
uteuzi wenu mliopewa na Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. PSPF ipo tayari wakati wote kushirikiana
nanyi katika kuleta tija katika utendaji wa Wizara ya Fedha na sekta nzima ya
Hifadhi ya Jamii kwa ujumla hapa nchini.
PSPF - Tulizo la Wastaafu
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni - PSPF
Usajili wa Okwi wazuiwa Yanga
Huku Ligi ya kandanda nchini
Tanzania ikitarajia kuanza mzunguko wake wa Pili Mwishoni mwa juma hili,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa
mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati
likisubiri ufafanuzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA).
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF
iliyokutana leo (Januari 22 mwaka huu) kupitia masuala mbalimbali,
imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi aliruhusiwa
kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.
Okwi ambaye aliingia mgogoro na
klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC
Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili
kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du Sahel
likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.
Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
Emmanuel Okwi ambaye aliwahi Kuichezea Simba kabla ya kuuzwa kwenye Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia,alikaribishwa kwa mbwembwe na hoi hoi nyingi wakati alipokuja kuanza kuichezea Yanga mwishoni mwa mwaka uliopita ambapo katika mechi dhidi ya Simba alifunga bao 1 la kufutia machozi WAKATI Yanga ilipobamizwa bao 3-1 na Simba katika Mechi maalum kati ya watani hao wa jadi katika Soka la Tanzania.
Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.
Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
Emmanuel Okwi ambaye aliwahi Kuichezea Simba kabla ya kuuzwa kwenye Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia,alikaribishwa kwa mbwembwe na hoi hoi nyingi wakati alipokuja kuanza kuichezea Yanga mwishoni mwa mwaka uliopita ambapo katika mechi dhidi ya Simba alifunga bao 1 la kufutia machozi WAKATI Yanga ilipobamizwa bao 3-1 na Simba katika Mechi maalum kati ya watani hao wa jadi katika Soka la Tanzania.
MAN UNITED YABANDULIWA NJE NA SANDERLAND
Baada ya muda wa kawaidia United ilikuwa ikiongoza kwa goli moja kwa bila, lakini kuwa walipoteza mechi ya awamu ya kwanza kwa magoli mawili kwa moja, mechi hiyo ilibidi kuongezwa dakika thelathini zaidi za ziada.
Katika muda huo wa ziada Sunderland nusura ifuzu moja kwa moja lakini sherehe hizo zilikatizwa baada ya dakika moja pale United iliposawazisha kupitia kwa nyota wake Chicharito, na hivyo kufanya timu hizo mbili kutoshana nguvu ya jumla ya magoli matatu kwa matatu bada ya dakika mia moja na Ishirini.
Mechi hiyo iliamuliwa kupitia mikwaju ya penalti na kwa mara ya kwanza, makipa wa timu hizo mbili waliokoa mikwaju kadhaa.
Kwa Ujumla mikwaju saba ziliokolewa au kupigwa nje na hivyo Sunderland kujikatia tikiti ya fainali dhidi ya Manchester City kwa magoli mawili kwa Moja.
Fainali ya kombe hilo itachezwa tarehe mbili Machi mwaka huu katika uwanja wa Wembley.
ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE, SAID RAMADHANI BWANAMDOGO AFARIKI DUNIA
Picha ya enzi za uhai wake aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Marehemu Said Ramadhani Bwanamdogo
0 maoni:
Post a Comment