Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Friday, May 27, 2011

BANZA STONE ATAMBULISHWA RASMI EXTRA BONGO




Na Rachel Mwilligwa,Dar es Salaam


HAYAWI HAYAWI, yamekuwa, ndivyo unavyoweza kusimulia utambulisho rasmi wa

mwanamuziki nguli nchini,Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ ndani ya bendi ya Extra Bongo jana katika ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Hii ilikuwa ni shoo isiyohitaji kusimuliwa lakini kwa waliokosa bahati ya kuhudhuria shoo hiyo waombe Mungu awape fursa siku nyingi wahudhurie na kumuona Mwana Massanja, Mwalimu wa Dunia, Banza Stone kama ataweza kuwapagawisha kama alivyofanya katika utambulisho.


Unajua ni kwanini, Hebu sikia ilivyokuwa, Banza alipanda rasmi jukwaani saa 6.37 na kusalimia mashabiki na wadau wake waliokuwa wamejitokeza kushuhudia shoo hiyo ya Extra Bongo sambamba na utambulisho wake na kama ilivyo kawaida yake alianza kushambulia jukwaa kwa kibao maalum cha utambulisho cha ambacho alikiita ‘ Watu na Falsafa ya Maisha’


Ilimchukua takribani nusu saa kuwatendea vema mashabiki wake mpaka alipoamua kushuka jukwaani saa 7.04 huku akipagawisha vema kwa vibao kadhaa kama kile cha Elimu ya mjinga ni majungu kilichowafanya mashabiki kuinuka vitini na kujumuika vema na burudani ya bendi hiyo.


Kama kuna wadau wa muziki wanadhani Mwana Masanja ni mhuni, basi watakuwa wamekosea sana kwani mavazi yake yalitosha kumtambulisha vema uhalisia wake baada ya kuwa na viwalo vya uhakika.


Alipandaa jukwaa akiwa na suti nyeupe ‘fuluuuu’ ikichombezwa na shati la rangi jekundu lililomfanya aonekane vema ukumbini hapo hasa nyakati za usiku huku akinogesha viwalo hivyo na ususi wake wa nyele za kwenda nyuma zenye staili ya mbinjuo.


Mbali ya kutambulishwa kwa Masanja, pia bendi hiyo ya Extra Bongo ilizindua rasmi blog yao inayokwenda kwa jina la WWW. Extrabongo.blogspot.com pamoja na Meneja wa bendi, Tito Thomas.


Hii ilikuwa ni story fupi kuhusiana na utambulisho wa Banza Stone, fuatilia hadithi kamili punde………..


0 maoni:

Post a Comment