Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Saturday, April 25, 2015

HONGERA ANGEL MICHAEL MACHELLAH KWA KUPATA KIPAIMARA LEO.

 Askofu msaidizi  wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe (Kulia) akizungumza na Watoto waliopata Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katholiki la Kimara jijini Dar es Salaam. 
 Mtoto Angel Machellah(mbele) akiwa na watoto wenzie wakijiandaa kuingia kanisani wakati wa kupokea Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Parokia ya Kimara Dar es Salam. 
 Angel akiwaongozwa wenzake kuingia Kanisani.

Thursday, April 23, 2015

UBA YAZINDUA HUDUMA YA U- MOBILE TANZANIA.

 Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Unite Bank of Afrika(UBA), Generali Mstaafu, Robert Mboma(kushoto) na Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo, Demola Ogunfeyimi(wa pili kushoto) wakipongezana mara baada ya kuzindua huduma mpya ya U-mobile kwa benki hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana.Kushoto ni  Meneja wa Benki hiyo Nchini Tanzania, Dinko Svetic na Mkuu wa Oparesheni wa Benki hiyo, Chis Byaruhanga wakipiga makofi na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mauzo na masoko wa benki hiyo, Julius Konyani. 
 Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Unite Bank of Afrika(UBA), Generali Mstaafu, Robert Mboma akikata utepe kuashira uzinduzi huo.
 Wasanii wakicheza wakati wa uzinduzi huo.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki hiyo na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.
 Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo, Demola Ogunfeyimi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

BENKI ya UBA Tanzania (United Bank for Africa) leo hii imezindua huduma mpya ya U- Mobile katika ofisi zao kuu jijini Dar es Salaam. Wateja wa Benki hiyo wanaweza kupata huduma hiyo mara moja kwa kujiandikisha na kupata huduma kwenye simu ya mkononi na vifaa vya umeme.
UBA ni Benki ya kwanza kuwa na huduma yake ya simu kupatikana katika katika majukwa 2 tofauti: kupitia App ya simu ya mkononi kwa wale ambao wana smart phone na pia kupitia mfumo wa USSD code, ambayo inapatikana kwa watu wote kwa kujisajili kupitia *150*77#.
Kwa kutoa huduma ya U- Mobile, Benki hiyo inawapa wateja wake njia rahisi ya kupata na kusimamia fedha zao. Pia kupitia U- Mobile wateja wa UBA watapata zaidi ya huduma 14 zikiwemo; uhamisho wa fedha, usimamizi wa fedha, kununua salio, kulipia huduma za: LUKU, DSTV, kununua tiketi nk.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Tanzania, Demola Ogunfeymi, alisema, “Tunafurahi sana kuweza kuwapa watanzania huduma hii kwa mifumo ambayo inawafa, nia yetu ni kuwapa wateja wetu suluhisho bunifu na rahisi la kuwawezesha kusimamia fedha zao”.
Naye Mwenyekiti wa UBA Tanzania, Jen. Robert Mboma, alisema, “Nia ya benki hii kutoa na kuhakikisha bidhaa na huduma kwa wateja ni ya kipekee na ni ya hali ya juu”.
Mkuu wa Bidhaa wa UBA Tanzania, Julius Konyani alisema kwamba benki hiyo imeweka mikakati ili kuhakikisha akaunti za wateja zinabaki salama. Aliendelea kusema, “Tuna timu ambayo inawajibika na usimamizi wa huduma ya U- Mobile na kutoa msaada masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki”.
Huduma hii inapatikana kwa wateja wetu ambao wana akaunti za XXX na Akiba au kadi ya UBA Prepaid na ni lazima kwanza wakamilishe fomu za kujiandikisha zinazopatikana katika matawi ya yote ya benki ya UBA. Mchakato huu ni wa haraka na rahisi kwani maelezo yote yanapewa kwa mteja ili aanze kutumia huduma hiyo haraka.
 Mkuu wa Mauzo na masoko wa benki hiyo, Julius Konyani akizungumza. 

Friday, March 27, 2015

SAFARI NYAMA CHOMA DAR ONE-TEMEKE JMAPILI WIKI HII.


Thursday, March 26, 2015

FEZA SCHOOL YATEMBELEA KIWANDA CHA COCACOLA JIJINI DAR ES SALAAM.


Mdhibiti wa ubora(Quality Controller) wa Kampuni ya Cocacola Kwanza, Kapalila Hamis akiwaonyesha kifaa maalum cha kutengenezea chupa za soda za plastiki, wanafunzi wa Darasa la saba wa Feza ya Mikwecheni jijini Dar es Salaam walipotembelea Kiwanda hicho.
Qulity Controller akiendelea kuwaonyesha kifaa hicho
 Mchanganyaji wa madawa wa Kiwanda cha Cocacola Kwanza cha  jijini Dar es Salaam akiwaelekeza jambo wanafunzi wa Fedha
 Cyrup Marker,Said akiwaelekeza

Kapalila akizungumza na wanafunzi hao

Kapalila akiwaelekeza jambo
 Kapalila akiwaelekeza namna chupa zinavyotengenezwa
 Kapalila akiwaonyesha unga maalum wa kutengenezea chupa za plastiki
 Water treatment wa maji ya Dasani akizungumza na wanafunzi hao jinsi anavyofanya kazi.
 Wanafunzi wa FEZA wakiwa na Lekopoz Shareacoke

 Wanafunzi wa FEZA wakitosi na Cocacola Bariiidi
 Mwanafunzi wa Feza akipata Cocacola Bariiiiiiiiiiiiidi

 Wanafunzi wa FEZA wakifurahi na Lekopoz


Le Kopoz

Thursday, October 30, 2014

SAFARI LAGER YAZINDUA RASMI PROGAMU YAKE YA “SAFARI LAGER WEZESHWA” KWA MSIMU IV, 2014.

 Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kushoto) akiwaonyesha kipeperushi cha shilingi 2200,000 000/= zitakazogawiwa kwa wajasiliamali wakati wa uzinduzi wa prpgramu ya Safari Wezeshwa msimu wan ne uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji wa programu hiyo, Joseph Mmigunda.
  KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imeziduwa rasmi programu yake ya Safari  Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa wajasiriamali wadogo wadogo Nchini.  

Akizungumza  na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo  alifafanuwa ya kwamba “ programu hii ni hazina tosha kwa wajasiriamali wadogowadogo nchini kwani itarahisisha kazi  kwa kuwepo na vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi”.

Programu hii ni msimu wa nne tangu kuanzishwa kwake na  imeleta mafanikio makubwa kwa wajasiriamali waliopata uthubutu wa kujaribu kujiunga na hatimae kuongeza uchumi wa nchi.

Bw. Oscar alifafanuwa kuwa, Programu hii itafanyika takribani mikoa yote Nchini ambapo fomu zitaanza kutolewa kuanzia leo kupitia mtandao wa www.wezeshwa.co.tz na baadae kusambazwa katika mabohari na viwanda vya TBL nchi nzima.Hii itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia kujaza fomu kwa usahihi na kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae waliokidhi nafasi zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi  pamoja na kukabidhiwa ruzuku  zao. 

Nae Jaji kutoka TABDS, Bwana Joseph Migunda alisema kuwa  “Zoezi hili linahusisha majaji wenye utaalamu na  wenye umakini  kwa namna moja au nyingine.Hivyo aliomba wajasiriamali wote wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye  malengo ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hii”.
Jaji wa programu Safari Wezeshwa kutoka Kampuni ya TABDS, Joseph Mmigunda(kulia)  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa program hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

RAIS KIKWETE AWASILI VIETNAM KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI.

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mhe Truong
Tan Sang wakikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake
wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya
kwanza ya ziara yake rasmi  ya siku mbili nchini humo leo Jumatatu
Oktoba 27, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua akishuhudiwa
na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam  wakati wa
mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya
ziara yake rasmi  ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa  na mwenyeji wake Rais Mhe
Truong Tan Sang wa Vietnam  wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu
ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi  ya siku mbili
nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu
Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong,
katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo
Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana baada ya
kutembelea kampuni ya mawasiliano ya VIETTEL Jumatatu Oktoba 27, 2014