Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Wednesday, June 13, 2012

Pazia la EBSS kufunguliwa kesho kutwa Dodoma



Na Mwandishi Wetu Dodoma
IKIWA kesho kutwa (Juni 16) ndio pazia la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS) linafunguliwa rasmi kwa kuanza kutafuta vipaji mkoani Dodoma ambapo maelfu ya  watu wameonesha nia ya kujitokeza kushiriki.
Mkoani hapa vijana wengi wameonesha kuwa na shauku kubwa ya kusubiria kushiriki katika usaili huo ambapo unaanza rasmi keshokutwa (Jumamosi ya Juni 16) katika ukumbi wa Royal Village.
Shauku hiyo inaweza kuwa inasababishwa na dau la zawadi la milioni 50 lililotangazwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel lakini pia dili la kuendelezwa kisanii ambalo nalo linawavutia vijana zaidi.
Akizungumzia usaili wa kesho kutwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampun ya Benchmark Production Ritha Paulsen alisema kuwa usaili wa mwaka huu watachukua washiriki kuanzia miaka 16 na kuendelea.
Alisema kuwa uamuzi huo wa kuchukua washiriki wa kuanzia miaka 16 ni kuwapa nafasi wale wenye uwezo wa kuimba na kupanga sauti ili nao wajaribu bahati yao.
“Najua kwa mwaka huu kwa kuwa shindano hili linadhaminiwa na Zantel hivyo mambo yamekuwa ni makubwa zaidi na napenda kuwaomba vijana kujitokeza kwa wingi zaidi kutumia fursa hii ambayo Zantel inawapatia mwaka huu” alisema Ritha.
Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Ali Bin Jarsh akizungumzia shindano hilo alisema kuwa Zantel inatambua nafasi ya muziki katika kukuza ajira na nchini.
Alisema kuwa Zantel imeamua kupitia Epiq Bongo Star Search kuinua vipaji vya vijana katika muziki ikiwa pamoja  na kuwatengenezea njia ya mafaniko.

0 maoni:

Post a Comment