Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onyesho kubwa la ijumaa la kuwaaga wapenzi na mashabikiki wa bendi hiyo litakalofanyika katika Ukumbi wao New White House Kimara jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kiongozi wa Bendi hiyo Rogath Hega wa Katapila
Na Mwali IbrahimBENDI ya muziki wa dansi ya Extra bongo 'Wazee wa kizigo' inatarajia kushiriki tamasha la muziki wa Afrika 'First Africa' linalofanyika kila mwaka nchini Finland.
Bendi hiyo inataondoka nchini Alfajiri ya Jumapili ijayo kwenda katika tamasha hilo kwa muda wa mwezi mmoja huku ikiwa na jumla ya Wanamuziki 15 na mfadhili mmoja.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alisema kwa mara ya kwanza bendi hiyo inashiriki katika tamasha hilo ambalo huwa linafanyika kila mwaka na huu ukiwa ni mwaka wa 11 tangu lianzishwe ambapo kwa mwaka huu katika bendi za Afrika watashiriki wao, Awilo longomba na bendi ya Zimbabwe.
Alisema, ushiriki wao katika tamasha hilo utadumu kwa miaka miwili kutokana na kusaini anano mkataba wa muda huo.
"Mwaka 2008 wakati nikiwa TOT bendi waliniita nikatoe burudani peke yangu lakini maswala ya Visa yalisumbua nikashindwa lakini kwa sasa wameniita tena pamoja na bendi yangu nafurahi kwani itanipa nafasi nzuri ya kuweza kujitangaza kimataifa," alisema.
Aliongeza kuwa katika msafara wake huo kwa upande wa Wanamuziki watakaoenda ni Ramadhani Mhoza 'Rama Pentagon', Michael Atanas 'atanas Muntanabe', Ally Choki na Rogert Hega 'Katapila, Wapiga vyombo ni Martin Kibosho, Oseah Mgoachi, Adam Hassan, Tomm Migula na Salum Issa.
Kwa upande wa wanenguaji ni Hassan Mussa 'Nyamwela, Isack Buruani 'Danger Boy', Otilia Bonifance, Angel Joshua na Lightness na Mdhamini wao Chief Kiumbe.
Aliongeza kuwa Ijumaa hii watafanya onesho maalum kwa ajili ya kuwaaga mashabiki wao ambalo litafanyika katika ukumbi wao wa New White house uliopo Kimara Korogwe ambapo sambamba na wao pia watakuwepo wasanii wa kizazi kipya Chid benz, Hussen Machozi, Q Chilla na Matonya.
Mkurugenzi akizungumza na waandishi wa habari
0 maoni:
Post a Comment