PATRICK NYANGUSI BINGWA WA SINGLES AFRIKA SAFARI POOL.
Wachezaji na
mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba
mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji
mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika
mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa
Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akicheza dhidi ya
mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini (hayupo pichani) wakati wa
mchezo wa fainali uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa
Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi (kushoto) akiwa na
mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini kabla ya kuanza mchezo wa
fainali uliofanyika jijini Blantyre nchini Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na
mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba
mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji
mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika
mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na
mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji
Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles)
Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na
mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji
Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles)
Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji wa
timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara
baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika
yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Mgeni
rasmi,Mjumbe wa Baraza la Michezo Nchini Malawi, Sharaf Pinto(wa pili kushoto)
akiwa na mabingwa wa Singles(mchezaji mmoja mmoja).Kutoka kulia ni mshindi wa
tatu kutoka Zambia, Moses Mofya,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen
Jagdev na Bingwa gwa Afrika kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi wakiwa katika
picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi medali zao Blantyre Malawi mwishoni
mwa wiki.
Mabingwa wa
Afrika wa mchezo wa pool wakiwa katika
picha nya pamoja.Kutoka kushoto ni Mshindi wa pili wa Afrika kutoka Afrika Kusini,Vishen Jagdev,Bingwa wa Afrika, Patrick
Nyangusi na mshindi watatu kutoka Zambia, Moses Mofya mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao jijini Blantyre
Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa
Afrika wa Safari Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akiwa katika picha ya
pamoja na warembo wa Blantyre Malawi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya medali
ya zahabu mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi
Wetu, Blantyre Malawi.
MCHEZAJI wa
timu ya Safari Pool Taifa, Patrick Nyangusi ameibuka Bingwa wa Afrika katika
mashindano ya mchezaji mmoja mmoja(singles) wanaume yaliyojumuisha timu saba
kutoka katika Nchi sita za Afrika.
Patrick
Nyangusi aliupata ubingwa huo kwa kumfunga mchezaji bora wa Afrika Kusini,
Vishen Jagdev 6-4,katika mchezo ambao ulisisimua wapenzi na mashabiki wengi wa
mchezo huo uliofanyika katika ukumbi wa kisasa wa Roben Complex jijini Blantyre.
Nyangusi kwa
ubingwa huo alizawadiwa medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili alichukua
mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini ambaye alizawadiwa Medali ya
Silver wakati mshindi wa tatu ni Moses
Mofya kutoka Zambia ambaye alimfunga mchezaji wa Tanzania, Omary Akida, 5-3 na hivyo
Moses Mofya kuzawadiwa Medali ya Fedha na nafasi ya nne ilichukuliwa na
mchezaji kutoka Tanzania, Omary Akida.
Upande wa
timu zilizowakilisha Nchi, Zambia waliibuka mabingwa katika mchezo ambao
uliendeshwa kwa mfumo wa ligi ambapo Zambia waliongoza kwa pointi 14.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na timu kutoka Nchi ya Afrika Kusini kwa pointi 12,na nafasi
ya tatu ilichukuliwa na Nchi ya Tanzania ambao walipata pointi 9, wakati nafasi
ya nne ilibaki kwa wenyeji Malawi ambao walipata pointi 4.
Akizungumza
Mkurugenzi wa mashindano ya AAPA (All Africa Pool Associations), Rick
Schoenlank, alizipongeza Nchi zote zilizoshiriki mashindano hayo,pili
aliwapongeza waandaaji wa mashindano kwa maandalizi mazuri na mwisho
aliipongeza Tanzania kwa kutoa bingwa wa Singles kwamwaka 2013.
Nae mgeni
rasmi aliyefunga mashinndano hayo, Mjumbe wa Baraza la Michezo la Nchini
Malawi, Sharaf Pinto, kwa niaba ya Waziri wa michezo wa Malawi,aliipongeza pia
Tanzania kwa kutoa bingwa Singles na kuwaomba Tanzania kuwa karibu na wachezaji
wa Malawi ili kubadilishana uzoefu na udugu pia kwa kutembeleana na kucheza
mechi za kirafiki.
Lakini pia
aliwapongeza Zambia kwa kutwaa ubingwa wa timu na vilevile aliwapongeza Malawi
kwa nafasi waliyopata si mbaya sana, ni nafasi ambayo inawafanya wajiandae
vyema kwa mashindano yajayo.
Mwisho
aliwapongeza kila Nchi kwa kuleta uwakilishi na kuwatakia safari njema ya
kurejea Nchini salama mpaka mashindano mengine mwakani.
Mashindano
ya mwaka huu yalijumuisha Nchi takribani 6, ambazo ni Afrika Kusini, Zambia,Tanzania,Lesotho,Namibia
na wenyeji Malawi 1 na Malawi 2.
Timu ya
Safari Pool ililiyokwenda Malawi ina jumla ya wachezaji 8, ambao ni Mohamed
Idd, Patrick Nyangusi Festo Yohana ,Mereczedec Amadeus,Omary Akida,Abdalah
Hussen ,Godfrey Swain a Nahodha Charles Vernas na viongozi watatu ambao ni
Meneja wa timu Nabil Hiza,Katibu wa chama cha pool Taifa, Amos Kafwinga na
Makamu Mwenyekiti, Fred Mush
Mashindano
ya AAPA mwakani yanatarajiwa kufanyika Tanzania jijini Dar es Saalaam.
0 maoni:
Post a Comment