Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Sunday, April 26, 2015

Chocky aipasua Twanga.

 Mwimbaji wa nyimbo za mziki wa dansi, Ally Chocky (katikati) akitambulishwa kwa wapenzi na mashabiki wa mziki huo wakati onyesho maalum la utyambulisho kwa wanamuziki watatu, Ally Chocky, mcheza shoo, Super Nyamwela na mpiga kinanda, Victor Mkambi.Onyesho hilo lilifanyika jana katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni Jijijini Dar es Salaam.Kulia ni Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Lwiza Nyoni na msaidizi wake Kalala Junior.
 Chocky akiwapungia mkono mashabiki mara baada ya kutambulishwa rasmi.
 Mcheza shoo na Rais wa wacheza shoo, Super Nyamwela akifunguliwa kwenye beki ili atambulishwe rasmi wakayi wa onyesho maalum la utambulisho lililofanyika katika Ukumbi wa Mango Garden Dar es Salaam jana.
 Super Nyamwela akicheza wakati wa utambulisho wake katika Bendi ya Twanga Pepeta
 Choki akiimba mara baada ya utambulisho rasmi nyimbo ya "Usiyempenda kaja" utunzi wake yeye mwenyewe.

Na Mwandishi Wetu.
UJIO na utambulisho wa wanamuziki watatu ndani ya Bendi ya Twanga Pepeta umeleta mpasuko mkubwa uliopelekea kwa baadhi ya wanamuziki wakongwe na wenyeji wa bendi hiyo kutopanda kabisa jana wakati wa utambulisho rasmi wa Aliyekuwa Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Chocky pamoja na aliyekuwa kiongozi wa wacheza shoo wake, Super Nyamwela kurudi Twanga Pepeta.
Ally Chocky, Super Nyamwela na Mpiga Kinanda, Victor Mkambi wametambulishwa rasmi jana katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam na kushangiliwa na maelfu ya wapenzi na mashabiki wa mziki wa Dansi huku baadhi ya wanamuziki nguli na wenyeji wa Bendi hiyo kukosekana jukwaani.
Ripota wetu alizungumza na wahusika pamoja na viongozi wa bendi hiyo ambapo kiongozi wa bendi hiyo, Lwiza Nyoni hakupatikana kwenye simu lakini kiongozi msaidizi, Kalala Junior alipatikana na kukiri kuwa kunatatizo upande wa uongozi lakini hilo ni la ndani na kesho jumatatu wanakikao ambapo wanatarajia kulimaliza haswa la muimbaji Saleh Kupaza, Rama Pentagoni yeye alisimamishwa na anatarajia kumaliza adhabu hiyo Mai 3,2015 wakati Kibosho yeye kaihama Bendi na sasa yuko katika Bendi ya Diamond Platinam.
Ripota wetu pia alizungumza na wanamuziki kujiridhisha ambapo Saleh Kupaza alithibitisha kuwa kunatatizo ndani ya uongozi na haswa Kiongozi wa Bendi, Lwiza Nyoni ambaye alimkataza asipande kabisa jana wakati wa utambulisho wa wanamuziki hao kwa sababu ambayo alitaja kuwa hajafanya mazoezi ya nyimbo mpya ya Ally Chocky.Lakini Kupaza alisema “tatizo si hilo tu, mimi na Kiongozi Lwiza tumekuwa na matatizo muda sasa na msimamo wangu najua ndio unao nigharimu Kupaza, nimekuwa na msimamo daima kwenye maslahi na maendeleo ya bendi lakini Lwiza yuko kiofisi zaidi yaani hajali na badala yake naonekana mbaya siamini kama ujioa wa hawa wanamuziki umemuongezea kiburi cha kufikia kunikataza kupanda jukwaani hilo sijui ila ninatatizo nae”.
Ripota alimuuliza kama wanatatizo lolote na Chocky, ambapo alisema Kupaza, “mimi sina matatizo na Chocky wala ujio wa mwanamuziki mwenzangu yeyote nampenda Chocky hata yeye naamini ananipenda na ujio wake najua tutasonga mbele lakini alisisitiza tena sina tatizo na mtu yeyote zaidi ya kiongozi wangu Lwiza na hayajaanza jana matatizo hayo”.
Rama Pentagoni yeye alithibitisha kuwa anatumikia adhabu na Kibosho yeye tayari kishaihama rasmi bendi hiyo ya Twanga Pepeta yuko na Diamond kwa sasa.
Ripota wetu hakuishia hapo alipanda kwa Mkurugenzi wa Bendi hiyo, Asha Baraka baada ya juhudi za Kiongozi wa Bendi, Lwiza Nyoni kutopatikana ambapo alisema swala hilo ni la kiutenjaji zaidi mwenye majibu sahihi ni Kiongozi wa Bendi Lwiza Nyoni ambaye kwa wakati huo alikuwa hapatikani katika simu yake ya mkononi.
Upande wa shoo kwa ujumla ilipendeza sana na ilikonga nyoyo za wapenzi na mashabiki wengi wa muziki wa dansi waliojitokeza kushuhudia utambulisho huo.
Zaidi kilicho konga nyoyo za watu ni nyimbo mpa ya Ally Choki ya Usiyempenda kaja pamoja na nyimbo nyingi za zamani ambazo waliziimba pamoja enzi hizo Chocky akiwa Twanga walizikumbushia.                  


Choki akicheza sambamba na wacheza shoo wakati wa utambulisho huo Mango Garden Dar es Salaam jana.
 Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Lwiza Nyoni akiimba wakati wa utambulisho wa wanamuziki hao Mango Garden jana.
Wacheza shoo wa kike wa bendi hiyo wakicheza wakati wa onyesho hilo.
 Chocky na Lwiza wakiimba kwa pamoja wakati wa onyeso hilo.
Wacheza shoo wakionyesha umahili wao.
 Kiongozi msaidizi wa bendi hiyo, Kalala Junior akiimba wakati wa onyesho hilo.
Wacheza shoo wakicheza. 
 Chocky na Rapa, Frenk Kabatano wakiimba wakati wa utambulisho huo.
 Wacheza shoo wakicheza. 
 Wacheza shoo wakicheza mbele ya mashabiki.

0 maoni:

Post a Comment