Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Thursday, April 23, 2015

UBA YAZINDUA HUDUMA YA U- MOBILE TANZANIA.

 Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Unite Bank of Afrika(UBA), Generali Mstaafu, Robert Mboma(kushoto) na Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo, Demola Ogunfeyimi(wa pili kushoto) wakipongezana mara baada ya kuzindua huduma mpya ya U-mobile kwa benki hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana.Kushoto ni  Meneja wa Benki hiyo Nchini Tanzania, Dinko Svetic na Mkuu wa Oparesheni wa Benki hiyo, Chis Byaruhanga wakipiga makofi na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mauzo na masoko wa benki hiyo, Julius Konyani. 
 Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Unite Bank of Afrika(UBA), Generali Mstaafu, Robert Mboma akikata utepe kuashira uzinduzi huo.
 Wasanii wakicheza wakati wa uzinduzi huo.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki hiyo na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.
 Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo, Demola Ogunfeyimi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

BENKI ya UBA Tanzania (United Bank for Africa) leo hii imezindua huduma mpya ya U- Mobile katika ofisi zao kuu jijini Dar es Salaam. Wateja wa Benki hiyo wanaweza kupata huduma hiyo mara moja kwa kujiandikisha na kupata huduma kwenye simu ya mkononi na vifaa vya umeme.
UBA ni Benki ya kwanza kuwa na huduma yake ya simu kupatikana katika katika majukwa 2 tofauti: kupitia App ya simu ya mkononi kwa wale ambao wana smart phone na pia kupitia mfumo wa USSD code, ambayo inapatikana kwa watu wote kwa kujisajili kupitia *150*77#.
Kwa kutoa huduma ya U- Mobile, Benki hiyo inawapa wateja wake njia rahisi ya kupata na kusimamia fedha zao. Pia kupitia U- Mobile wateja wa UBA watapata zaidi ya huduma 14 zikiwemo; uhamisho wa fedha, usimamizi wa fedha, kununua salio, kulipia huduma za: LUKU, DSTV, kununua tiketi nk.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Tanzania, Demola Ogunfeymi, alisema, “Tunafurahi sana kuweza kuwapa watanzania huduma hii kwa mifumo ambayo inawafa, nia yetu ni kuwapa wateja wetu suluhisho bunifu na rahisi la kuwawezesha kusimamia fedha zao”.
Naye Mwenyekiti wa UBA Tanzania, Jen. Robert Mboma, alisema, “Nia ya benki hii kutoa na kuhakikisha bidhaa na huduma kwa wateja ni ya kipekee na ni ya hali ya juu”.
Mkuu wa Bidhaa wa UBA Tanzania, Julius Konyani alisema kwamba benki hiyo imeweka mikakati ili kuhakikisha akaunti za wateja zinabaki salama. Aliendelea kusema, “Tuna timu ambayo inawajibika na usimamizi wa huduma ya U- Mobile na kutoa msaada masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki”.
Huduma hii inapatikana kwa wateja wetu ambao wana akaunti za XXX na Akiba au kadi ya UBA Prepaid na ni lazima kwanza wakamilishe fomu za kujiandikisha zinazopatikana katika matawi ya yote ya benki ya UBA. Mchakato huu ni wa haraka na rahisi kwani maelezo yote yanapewa kwa mteja ili aanze kutumia huduma hiyo haraka.
 Mkuu wa Mauzo na masoko wa benki hiyo, Julius Konyani akizungumza. 

0 maoni:

Post a Comment