Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Friday, June 12, 2015

WASHINDI WA PROMOSHENI YA KILI WAWASILI KUSHUHUDIA TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2015.


 
Baadhi ya washindi wa prpmosheni za Kilimanjaro waliowasili jijini Dar es Salaam kushuhudia  Kilimanjaro Tanzania Music Awards zinazotarajiwa kufanyka kesho katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Msham Isihakamwaka kutoka Mtwara, David Justin kutoka Mtawara na Robson Steven kutoka mkoani Mbeya.Tayari wako jijini Dar es Salaam kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro kesho.
 Msham(kushoto) na David wakiwa katika Hotel ya Kebby's ambapo washindi wote wameandaliwa kufikia kwa maandalizi ya kushuhudia Tuzo za Kill.

Na Mwandishi Wetu.
WASHINDI waliopatikana katika Promosheni za Bia ya Kilimanjaro zilizofanyika nchini kote wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo kushuhudia Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Hafla ya kukabidhi tuzo hizi inategemewa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi 13 June 2015.

Akizungumza na mwandishi wetu, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Bi. Pamela Kikuli amesema jumla ya washindi 22 wanatarajiwa kuwasili leo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania. Washindi hawa wataungana na washindi wengine 4 wa Hapa Dar Es Salaam. 

Bi. Pamela amesema washindi hawa walichaguliwa kwa njia ya kuponi baada ya wao kama wanywaji kununua bia ya Kilimanjaro kwenye Bar zilizokuwa na Promosheni. Washindi hawa wanalipiwa gharama zote za usafiri, Malazi na chakula kwa kipindi cha siku zote tatu watakazokuwa hapa jijini. 

Bi. Pamela amesema washindi wanaokuja ni kutoka katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Dodoma, Tanga, Mtwara, Mbeya, Kilimanjaro, Aruusha, Mwanza, Kahama, Musoma na Dar es Salaam.

TBL YAZINDUA BIA MPYA.

Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia boti ya kisasa iliyokuwa imebeba warembo wenzao na kinywaji hicho wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam. 
 
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakiwasili katika ufukwe wa Azura wakiwa na kinywaji hicho wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam.


 
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia mara baada ya wenzao kuwasili na boti ya kisasda ya kisasa iliyokuwa imebeba kinywaji hicho wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.Kulia ni waandishi wa habari wakiwa kazini.

 
Waremo wa kinywaji kipya cha Kill Twist wakishangilia mara baada ya wenzao kuwasili na boti ya kisasa ya kisasa iliyokuwa imebeba kinywaji hicho wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.



 
Picha ya pamoja ya moja ya wageni waalikwa na warembo wa kill twist mara baada ya uzinduzi.

 
Baadhi ya stafu wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) wakiwa katika picha ya pamoja na  kinywaji cha kill twist mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.



KAMPUNI ya Bia nchini (TBL) leo hii imezindua bia mpya ya Kilimanjaro Twist (Kili Twist) yenye ladha ya machungwa. Hii ni mara ya kwanza kwa bia ya aina hii yenye ladha ya matunda kuzinduliwa hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Twist Edith Bebwa alisema, “Leo hii TBL imebadilisha mtazamo wa watu wanvyoifikiria bia kwa kuzindua kinywaji hiki. Hii ni bia ya kwanza ya ladha ya matunda humu nchini na tunatarajia kuwafikia wateja wengine ambao wanataka kuhisi kama wanakunywa bia lakini kupata ladha iliyolaini na tamu zaidi na ladha halisi ya machungwa”.

Bia ya Kilimanjaro Twist ni bia yenye asili ya Kitanzania kwa 100% na ladha halisi ya machungwa, ina kilievi cha asilimia 2 % tu . Bia hii inatengenezwa hapa nchini kwa kutumia viuongo vyenye ubora na ni mwanafamilia wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ni kati ya bia bora zaidi nchini.

Bia ya Kilimanjaro Twist itauzwa kwa bei ya TZS 1,500/= na itapatikana katika baa na hoteli zote kubwa za Dar es salaam. Kutokana na mtindo wa kimiminika cha bia hii, mnywaji anapta kiburudisho cha hali ya juu na hivyo inawaruhusu wanywaji kuinywa hata mida ya chakula cha mchana, wakati wa mapunziko nyumbani au ufukweni kitu ambacho bia za kawaida haziruhusu.

“TBL imekuwa mstari wa mbele katika maswala ya uvumbuzi ya viwanwaji vyake na tumeendelea kufanya hivyo na bia hii ya Kilimanjaro Twist inadhibitisha hilo. Nawasihi wateja waijaribu Kilimanjaro Twist kwani ina ladha nzuri na inastahili katika tukio lolote” alimalizia kwa kusema.
 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(kulia) akizungumza na wajasiliamali pamoja na wakazi wa jijini Dar es Salaam waliojitokeza kwenye makabidhiano ya Ruzuku za Safari Lager Wezeshwa msimu wa nne yaliyofanyika Viwanja vya Leaders mwishoni mwa wiki.Kutoka kushoto ni Meneja mahusiano na mawasiliano Tbl, Emma Urio,Mkurugenzi wa taasisi ya wataalamu wa biashara(TBDS),Joseph Migunda na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.
 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(katikati) akimkabidhi mjasilamali, Neema Ulomi Cherehani za kisasa tatu katiaka hafla ya kuwakabidhi ruzu wajasiliamali waliofuzu vigezo katika program ya Safari Wezeshwa msimu wan ne.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.

 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(kushoto) akimkabidhi mjasilamali, Clemence Godfrey mashine ya kuchana na kukata mbao katiaka hafla ya kuwakabidhi ruzuku wajasiliamali waliofuzu vigezo katika program ya Safari Wezeshwa msimu wanne.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.
 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(wa pili kushoto) akimkabidhi mjasilamali, Frank Mashoko katiak hafla ya kuwakabidhi ruzuku wajasiliamali waliofuzu vigezo katika program ya Safari Wezeshwa msimu wanne.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(wa pili kushoto) akimkabidhi mjasilamali, Frank Mashoko katiak hafla ya kuwakabidhi ruzuku wajasiliamali waliofuzu vigezo katika program ya Safari Wezeshwa msimu wanne. Kutoka kushoto ni Meneja mahusiano Tbl, Emma Urio na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa

Picha ya pamoja

SAFARI LAGER YAJKABIDHI RUZUKU ZA WAJASILIAMALI MSIMU WA NNE KANDA YA NYANDA YA KASKAZINI


Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Adoh Mapunda(katikati) akimkabidhi, Amadeus Shayo mashine ya kusa nafaka wakati wa hafla ya kukabidhi ruzuku za Safari Lager Wezeshwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.

SAFARI LAGA YAKABIDHI RUZUKU ZA WAJASILIAMALI KANDA YA ZIWA KATIKA PROGRAMU YAKE YA SAFARI WEZESHWA.

 
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Baraka Konisaga(wa pili kushoto) akimkabidhi mjasiliamali Jenereta wakati wa hafla ya kukabidhi Ruzuku kwa wajasiliamali 10 wa Kanda ziwa katika Programu Programu ya Safari Wezeshwa msimu wa nne inayoendeshwa na Bia ya Safari Lager.Kutoka kulia ni Mratibu wa program hiyo kutoka Kampuni ya TABDS, Veronica Mwamunyange, Maneja matukio wa Tbl Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa.

Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Bia nchini kupitia Bia yake ya Safari Lager imekabidhi Ruzuku kwa Wajasiliamali 10 wa kanda ya Ziwa katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Furahisha mwishoni mwa wiki.
Wajasiliamali 10, waliokabidhiwa ruzuku hizo ni sehemu ya wajasiliamali 55 watakaowezeshwa nchini nzima katika Programu ya Safari Wezeshwa inayoendeshwa na Kampuni ya Tbl kupitia kinywaji chake cha Safari Lager.
Akizungumza na Wajasiliamali pamoja wageni waliojitokeza kwenye hafla ya makabidhiano ya Ruzuku hizo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga aliipongeza TBL, kupitia bia yake ya Safari Lager, kwa ubunifu mkubwa wa kuandaa program hii maalum ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo katika kuwainua kiuchumi inayojulikana kama “Safari Lager Wezeshwa”. Hivyo basi kuongeza fursa za ajira hapa nchini kupitia Ujasiriamali.  

Aidha Mkuu wa Wilaya aliwapongeza sana Wajasiriamali wote walioshiriki katika Programu  hii. Mvuto wa Wananchi wengi    kupenda    kuwa   Wajasiriamali   ni   jambo   jema, kwani litasaidia  sana  kukua  kwa  Sekta  Binafsi ambayo tunataka iwe Injini ya kuongeza ajira na Ukuaji wa Uchumi wetu.  Hivyo, nawapongeza sana na kuwatakia mafanikio Zaidi. 

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa  aliwapongeza sana wajasiriamali waliofuzu katika programu ya “Safari Lager Wezeshwa” msimu huu wa nne. Jumla ya ruzuku za vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 220,000,000/= vitagawiwa kwa wajasiriamali 55 katika kanda nne za Tanzania. Kwa kanda hii ya Ziwa, tutashuhudia wajasiriamali 10 wa kanda hii wakikabidhiwa ruzuku zao na mgeni rasmi. 

Ruzuku hizi zinazotolewa katika program ya “Safari Lager Wezeshwa” msimu huu wa nne zinafanya jumla ya ruzuku zilizotolewa kufikia 620,000,000/=. Jumla ya wajasiriamali 157 wamefaidika moja kwa moja na programu hii, wananchi wengine wengi wanafaidika kutokana na wajasiriamali hawa kukuza biashara zao. Jumla ya ajira mpya kwa watanzania 361 zinategemewa kuongezeka hadi kufikia mwisho wa msimu huu wa nne. Hili ni ongezeko lao la ajira kwa asilimia 116%. 

Mwisho kabisa alitoa wito kwa wajasiriamali wote waliofaidika na mpango huu kuzingatia vizuri malengo ya program hiyo. Wafanye kazi kwa bidii na kujituma, maendeleo na kukua kwa biashara zao kuwanufaishe wao wenyewe, na jamii inaowazunguka. 

Kwa wajasiriamali ambao hawajafuzu msimu huu, wasikate tamaa, washiriki tena kwa kujaza fomu mapema na kwa usahihi msimu ujao. Wajasiriamali wanaofuzu wanapatikana bila upendeleo wowote na hawa wanaopokea ruzuku zao leo hapa ni mashahidi wetu katika hilo.

HUAWEI INAENDELEA KUJIKITA KATIKA SECTA YA ICT NCHINI TANZANIA

 Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Tanzania Peter Zhang, akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwekezaji katika Tekinolojia ya ICT nchini.Mazungumzo hayo yalifanyika Makao makuu ya HUAWEI Tanzania jijini Dar es Salaam.
 
 
Tarehe 18 na 19 Juni 2015, ndani ya ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) uliopo mkoani Dar es Salaam, kampuni ya Huawei Tanzania itashirikiana na Wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kufanya kongamano la sekta ya Teknolojia ya IT. Kongamano hili litazungumzia teknolojia mpya ya IT ikiipa kipaumbele sekta mpya ya kuhifadhi data kwa kutumia njia ya mawingu.

Lengo na dhumuni ya kongamano hili ni kuendelea kuwawezesha Watanzania kwa njia moja au nyingine kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

kila mmoja wetu anaelewa  kua kwenye karne hii ya mawasiliano; teknolojia ya habari na mawasiliano ni muhimu sana hususani katika shughuli zetu za kila siku ziwe za kibinafsi au za kibiashara .

Kwa kupitia teknolojia ya Habati na Mawasiliano, dunia inakua zaidi na zaidi huku viwanda vilivyopo vikihitaji  kuhakikisha biashara inaendeshwa

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imewezesha kwa kiasi kikubwa ukuaji wa sekta mbalimbali na kufanya ongezeko la uvumbuzi wa vitu mbalimbali na hivyo kupelekea kuongezeka kwa mahitaji ya ajira  hususani kwa upande wa vijana
Huawei Technologies Tanzania co. Ltd, imekua katika kiini cha mzunguko wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ulimwenguni ; ikiendesha shughuli zake katika kila nchi mbalimbali duniani. Huawei imejizatiti huku kuhakikisha kua kiongozi kwenye uvumbuzi wa teknolojia mpya pamoja na ukuaji na ongezeko la maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo, viwanda, biashara, ...... n.k

Kampuni ya Huawei Tanzania imewekeza nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa na haswa  kwenye ukuaji wa maendeleo ya sekta ya Habari na Mawasiliano nchini. Katika sekta hii ya Habari na Mawasiliano, kampuni ya Huawei Tanzania imelenga Zaidi kwenye upande wa elimu na mawasiliano na imeahidi kuendelea kufanya hivo.

 

Mwaka 1998, Kampuni ya Huawei Tanzania ilianza shughuli zake nchini Tanzania na mpaka hadi leo ina wafanyakazi Zaidi ya 315 kupelekea kufanya idadi ya watanzania kua na Zaidi ya asilimia  75. Toka ianze shughuli zake za kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, Kampuni ya Huawei Tanzania imekua ikishikiriana na wadau wengine mbalimbali wa ICT ikiwemo  mashirika binafsi, mashirika ya uma pamoja na Serikali ya Tanzania.

Kampuni ya Huawei Tanzania inaongoza katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania na imekua ikishirikiana na wadau wengine wa mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel na TTCL katika kuchangia ukuaji wa mmoja mmoja kwenye hii sekta (ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

TBL YAZINDUA MUONEKANO MPYA WA KINYWAJI CHAKE CHA REDD’S ORIGINAL.

 Meneja wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL), Calvin Martin na Meneja wa Kinywaji cha Redd’s Original, Victoria Kimaro wakionyecha muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho kwa wafanyakaji iliyofanyika Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam





 Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imezindua muonekano mpya wa kinywaji hicho ambacho kinapendwa na wanywaji wengi kutokana na ubora wake na ladha yake nzuri ya apple.  

Akizungumza na Wafanyakazi wa TBL, Dar es Salaam  wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original, Victoria Kimaro alisema leo tunazindua muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original kikiwa kwenye chupa bila kubadilisha chochote ndani yake ambapo itabaki na ubora  ulele,ladha ileile ila muonekano mpya ambao utawavutia wapenzi wa kinywaji hicho Zaidi. 

Alisema Victoria, muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original wa kwenye chupa utakuwa kwenye ujazo wa mililita 375 na kopo mililita 330 ambao utavutia wateja wengi wa kinywaji hicho.  

Kimaro alisema “Nia kubwa ni kuhakikisha tunampa mteja thamani yake halisi pale atakapokuwa anatumia kinywaji cha Redd’s Original na tunaendelea kuwahakikishia ubora wake utabaki kuwa wa kiwango cha juu kama ilivyo kawaida yetu,”. 

Meneja,Victoria aliomba wanywaji wa  Redd’s Original waendelee kukitumia kinywaji hicho kwani ni kinywaji bora zaidi kwa sasa kinachompa mteja nafasi kubwa ya kumthamini na kuutambua mchango wake.

0 maoni:

Post a Comment