Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo akiimba wakati wa onyesho maalum katika Ukumbi wa Villa jijini Mwanza
Muimbaji,Redo Mauzo akiimba wakati wa onyesho hilo
Muimbaji wa Bendi hiyo,Banza Stone akitunzwa wakati akiimba kwenye shoo hiyo
Muimbaji wa zamani wa Bendi hiyo,Mwenzingo akikumbushia enzi zake
Kiongozi wa Bendi,Rogati Hega akiima wakati wa shoo hiyo
Muimbaji wa Bendi hiyo,Amina Kimobitel akiimba
Chocky akiimba
On
0
comments
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bi Ziporah
Pangani akimkabidhi kiongozi wa kundi la Abakambamoi Bw Projestus
Boniface kitita cha shilingi laki 5 ikiwa zawadi ya mshindi wa kwanza
wa fainali za mashindano Ngoma za Asili kwa Mkoa wa Kagera, katikati ni
Afisa utamaduni Manispaa ya Bukoba Evarisia Ruafiyami na Meneja masoko Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa Bw Andrwe Mmbwambo,Mashindano ambayo
yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra
Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
Baadhi
ya Wakazi wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera ambao walijitokeza kwa wingi
katika viwanja vya kaitaba kushuhudia fainali za Ngoma za Asili kwa Mkoa huo
ambyo mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa
.
Wasanii wakiwa kazini katika fainali za Ngoma za Asili kwa Mkoa huo ambyo
mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia
yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bi Ziporah
Pangani akimkabidhi kiongozi wa kundi la Ruau Bw Ezekhiah Henriko kitita
cha shilingi laki 6 ikiwa zawadi ya mshindi wa kwanza wa fainali za
mashindano Ngoma za Asili kwa Mkoa wa Kagera, katikati ni Afisa utamaduni Manispaa
ya Bukoba Evarisia Ruafiyami na Meneja masoko Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
Kanda ya Ziwa Bw Andrwe Mmbwambo,Mashindano ambayo yalidhaminiwa na kampuni ya
Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager bia ya Kanda ya Ziwa.
KUNDI la ngoma za asili la Ruau
limefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya ngoma mkoa wa Kagera chini ya
udhamini wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia kinywaji chake cha BALIMI EXTRA LAGER.
Kundi la Ruau limetwaa ubingwa huo
baada ya kupata alama 249 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi.600,000/= na
tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Kagera katika fainali za mashindano ya Kanda
yanayotarajiwa kufanyika julai 20 mwaka huu jijini Mwanza.
Washindi wa pili katika
mashindano hayo ni kundi la Abakambamoi ambao wamepata alama 227 na hivyo
kujinyakulia fedha taslimu shilingi 500,000/=nafasi ya tatu imechukuliwa na
kundi la Rugomoire kwa alama 226 na kuzawadiwa shilingi.400,000/= huku kundi la
Aruta wakiondoka na nafasi ya nne na kuzawadiwa shilingi 300,000/= .
Jumla ya vikundi 12 vimeshiriki
mashindano hayo,ambapo vikundi vingine vilivyo shika nafasi ya 5 mpaka 12
vimeondoka na kifuta jasho cha fedha taslimu sh.150,000/=
Mgeni rasmi katika mashindano
hayo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Ziporah Pangani akizungumza na washiriki wa
mashindano hayo pamoja na wakazi wa Mkoa wa Kagara waliojitokeza kushuhudia
fainali hizo ameipongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi
Extra Lager kwa kudhamini mashindano mbalimbali na kuvitaka vikundi vilivyo
shika nafasi ya kwanza vya Ruau kutoka Karagwe na kundi lililo chukua nafasi ya
pili la Abakambamoi kutoka Muleba kwenda kuwakilisha mkoa wa Kagera vema katika
mashindano hayo ya Kanda.
Ziporah amesema ni aibu kwa mkoa huo
kuwa wasindikizaji katika mashindano hayo na kuwataka maafisa utamaduni na
viongozi wa vikundi hivyo kuhakikisha kuwa wanafanya mazoezi kuanzia sasa
ili viweze kurejea na nafasi za juu katika katika mashindano hayo “
nawataka mreje mkiwa nafasi za juu ya kwanza mpaka ya tatu msipo pata nafasi
hizo hamto panda meri kurejea kagera”alisema Mkuu wa Wilaya huyo.
Naye Meneja masoko wa Kampuni
ya Bia Tanzani (TBL) Kanda ya Ziwa Andrew Mbwambo amesema kuwa kampuni
yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini shughuli mbalimbali za kijamii
ikiwemo michezo na burudani ikiwa ni shukrani zao kwa jamii kwa kutumia bidhaa
zao ambapo ameiomba jamii ili kampuni hiyo iweze kuendelea kudhamini shughuli
hizo wawaunge mkono kwa kutumia bidhaa zao, hasa bia ya Balimi Extra Lager bia
ya Kanda ya Ziwa pekee.
Aidha Mbwambo amewataka wakazi wa
jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi jumamosi hii kushuhudia mashindano hayo ya
ngoma za asili na kuwaona wawakilishi wao watakao wawakilisha katika mashindano
ya Kanda ambayo yatashirikisha mikoa 6 ya kanda ya ziwa ambapo pia amepongeza
mwitikio wa wakazi wa Kagera katika shughuli hiyo.
Vikundi vingine ambavyo vimeshiriki
katika fainali hizo ni pamoja na Rumanyika kutoka Karagwe, Bikolwengonzi kutoka
Bukoba, Tuelimishane kutoka Misenyi, Abasubi kutoka Biharamuro, Jipemoyo
Muleba, P. gaigwa, Abaligambo kutoka Bukoba na Obumoi ngonzi .
0 maoni:
Post a Comment