Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Wednesday, July 24, 2013

MWANALYAKU-MWANZA MABINGWA BALIMI NGOMA KANDA YA ZIWA 2013.

 Mabingwa wa Mashindano ya Ngoma Kanda ya Ziwa yanayojulikana kwa Balimi Ngoma Festival 2013,kikundi cha Mwanalyaku kutoka Wilani Magu Mkoani Mwanza wakishangilia na Kombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Polisi Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Kiongozi wa Kundi la Mwanalyaku kutoka Wilayani Magu Mkoani Mwanza akikabidhiwa Kombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za ngoma zinazojulikana kwa Balimi Ngoma Festival 2013 zilizofanyika katika Uwanja wa Polisi Mabatini jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
 Mpiga Ngoma kutoka kikundi cha Mwanalyaku cha Magu Mkoani Mwanza akipiga Ngoma kwa hisia kali.
 bBaadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakishuhudia fainali za mashindano ya ngoma Kanda ya Ziwa zilizojumuisha vikundi 10 kutoka Mikoa 5 ya Kanda ya Ziwa, Tabora,Shinyanga,Kagera,Mara na Mwanza
 Kundi la Ngoma la Egumba kutoa Mara wakicheza
 Kundi la Ngoma la Magereza kutoka Tabora wakicheza wakati wa fainali hizo
 Kundi la Ngoma la Mwanajilungu kutoka Shinyanga wakicheza
 Mpiga Ngoma wa Kundi la Mwanalyaku kutoka Magu ambao waliibuka mabingwa katika fainali hizo akitamba
 Meza Kuu wakishuhudia fainali za mashindano hayo
 Baadhi ya wakazi wa Mwanza wakishuhudia fainali hizo zililizokuwa za kusisimua
 
 Kundi la Egumba wakionyesha mambo yao
 Kundi la Mwanalyaku wakionyesha umahili wa kucheza na nyoka
 Hwa jamaa balaa
 Kundi laRugu kagera wakicheza
 Rugu Kagera wakionyesha mambo yao
 Duh
 Kiongozi wa Kundi la Mabuloh ya Jeshi kutoka Mkoa wa Shinyanga wakifanya vitu vyao
 Hao ndio mabuloh ya Jeshi ndani ya Uwanja wakitoa shoo
 Kundi la Ngoma la Abagambakamo kutoka Kagera wakicheza
 Duh hao ndio Mabuloh ya Jeshi kutoka Shinyanga ambao walitoa burudani ambayo kila mtu alifurahi
 Mabuloh ya Jeshi hao-Shinyanga
 Ngoma ya Litungu ikiwapagawisha wakazi wa Mara wakati wa fainali hizo
 Balaaa
Watu lukuki wakiwa wamejaa kushuhudia mashindano
 Umati wa watu wengi wakishuhudia fainali za mashindano ya Balimi Ngoma Kaanda ya Ziwa 2013.
 Mgeni rasmi wa hafla futari iliyoandaliwa na Benki ya BancABC kwa wafanyakazi wa makampuni mbalimbali, Sheikh Ismail Mohamed Salim akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel Kempisk Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Benki ya BancABC wa kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni na taasisi Bwana Zulfikar Chandoo akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Kempisk Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
Wageni waalikwa wakipata futari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akifuturu wakati wa hafla hiyo
BENKI ya BancABC leo hii imeandaa hafla fupi kujumuika kwa pamoja na wateja wake waliofunga katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kupata futari. Hafla hii fupi imefanyika jijini Dar Es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro na imehudhuriwa pia na Sheikh Ismail Mohamed Salim ambaye alikuwa mgeni wa rasmi.

Akizungumza katika hafla hii Meneja wa Benki ya BancABC wa kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni na taasisi Bwana Zulfikar Chandoo alisema kwamba, “BancABC tunathamini mchango mkubwa tunaopata kutoka kwa wateja wetu na tumeandaa hafla hii fupi ili kujumuika nanyi jioni hii ya leo ili kupata futari. Kwa kupitia mkusanyiko kama huu, tunadumisha mahusiano yetu ya kibiashara, tunajiweka karibu zaidi na marafiki, jamaa na ndugu zetu bila kujali tofauti zetu za kiutamaduni, imani au kidini”.

Mgeni rasmi wa hafla hii Sheikh Ismail Mohamed Salim aliwapongeza sana benki ya  BancABCkwa kutambua mchango wa wateja wake wanaofunga na kujitolea kuandaa shughuli hii. Aliwaasa waislamu kumkumbuka Mungu katika shughuli zao za kila siku kwani huo ndio mwanzo wa mafanikio katika biashara na shughuli nyinginezo za binadamu. Aliongeza pia, “ Tukio kama hili la Futari, linatupa nafasi ya kuungana na kutambua mchango muhimu ambao jumuiya ya kiislamu umetoa kwenye Historia na Urithi wa nchi yetu nzuri ya Tanzania.

Bwana Zulfikar alimalizia kwa kusema, “Tunapenda kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuchagua BancABC, tunapenda pia kuwakumbusha wateja wetu watakaosafiri kwenda Macca kwa ajili ya Hijja mji wa Mecca mwezi October mwaka huu, wafike kwenye ofisi zetu ili wajipatie kadi za VISA za kusafiria. Kadi hii ni njia salama na kusafiri na fedha zako popote uendapo. Unaweza kujipatia aidha kadi ya malipo ya kabla ya BancABC VISA cash card au kadi maalumu za kusafiria za BancABC VISA Travel Money. Kadi hizi ndio njia salama na rahisi ya kubeba fedha pale mtu anaposafiri nje ya nchi na dunia nzima kwa ujumla”. Aliongezea kuwa, BancABC ina huduma kabambe ya Kutoa mikopo wa Wajasiriamali kwa vigezo nafuu zaidi, ambapo wafanya biashara wadogowadogo wanaweza kujipatia mikopo ya kukuza biashara zao haraka na kwa urahisi zaidi kwani mfanyabiashara haitaji kuweka dhamana yoyote ili kupata mkopo huo. Tafadhali fika kwenye moja kati ya matawi yetu ya BancABC yaliyopo Dar es Salaam na Arusha ili upate maelezo zaidi na uanze kunufaika na huduma za BancABC.
Baadhi ya Wafanyakazi wa BancABC wakipata futari wakati wa hafla hiyo

0 maoni:

Post a Comment