Lori lenye namba za usajili T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka na kuziba njia
Lori likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika
Magari yakipita kwa shida baada ya Lori kudondoka
Askari wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika
Dereva wa gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika kifo
Wakichangamkia kuchota mafuta
YALE YALE!!! Wananchi wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ... bila kujali kama yaweza kulipuka
Wananchi Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka
Askari wa zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji
Wananchi mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota
Wakina mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada ya ajali
Kushoto ni Tingo Saimoni Msovela (23) na dereva wake Hassan Abdi wakijitahidi kuziba mafuta yasiendelee kuvuja
Tingo wa Lori hilo la mafuta baada ya kuokolewa kutoka kwenye Gari.
Ezekiel Kamanga
Watu wawili wamenusurika kifo baada ya roli la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya Scania walilokuwa wakisafiria kutoka Dar Es Salaam kwenda Zambia kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa Mbalizi barabara Mbeya Tunduma.
Dereva ametambuliwa kwa jina la Hassan Abdi 35 na msaidizi wake SaimonSovela 23 ambao walikuwa wametokea Dar es Salaam kuelekea Zambia likiwa limejaa shehena ya mafuta
Kwa mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.
On 0 comments
Waziri wa Ofisi ya Rais Menejmenti ya utumishi wa Umma na Mbunge wa jimbo la Ulanga Mh Celina Kombani Akipokelewa katika moja ya banda la maonyesho ya nanenane mkoani morogoro.Waziri huyo leo ametembelea mabanda tofauti kujionea shuguli za wakulima katika mabanda tofauti mjini morogoro leo
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mh Said Amanzi akiwa ameambatana na waziri katika maonyesho hayo leo mjini morogoro
MBUNGE WA MOROGORO KUSINI AHAMASISHA WANANCHI KATIKA SHUGULI ZA MAENDELEO
Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mh Innocent Kalogeris akifyatua matofali jana katika kata ya Kisemo Morogoro vijijini ikiwa ni siku aliyojipangia na wananchi wa jimbo hilo na yeye kama mbunge wao kuhamasishana kujitolea katika shuguli za maendeleo.
Mbunge huyo akionyesha mfano Namna ya kufyatua matifali.
Kata ya kisemo Morogoro vijijini inayoundwa na vijiji vitano navyo ni Nige ,Dabwala.Nige Mashariki,Nige Magharibi Nige Mteremko wamejipanga kufyatua tofali laki moja kwa ajili ya ujenzi wa shule na zahanati
Mbunge wa Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris akiendelea na shuguli ya kufyatua matolai jimboni kwake akishirikiana na wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris akiwa na mwenyekiti wa kijiji Mzee Dimoso wakati wa shuguli za kujitolea kijijini hapo
Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris akiongea na wananchi wa vitongoji vya Nige ,Dabwala.Nige Mashariki,Nige Magharibi Nige Mteremko
Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini pamoja na wananchi wa jimbo hilo wakiandaa udongo kwa ajili ya maandalizi ya kufyatua matofali jimboni kwake
On 0 comments
Ofisa Habari wa Kampuni ya Startimes Erick Cyprian kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezaka kwa chanal wakati wa kipindi hiki cha kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe kampuni hiyo kulia ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Zuhura Hanif Picha na SUPER D |
Ofisa Habari wa Kampuni ya Startimes Erick Cyprian kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezaka kwa chanal wakati wa kipindi hiki cha kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe kampuni hiyo kulia ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Zuhura Hanif Picha na SUPER D |
Ofisa Habari wa Kampuni ya Startimes Erick Cyprian kushoto akizungumza kwa msisitizo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuongezaka kwa chanal wakati wa kipindi hiki cha kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe kampuni hiyo kulia ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Zuhura Hanif Picha na SUPER D |
Ofisa Habari wa Kampuni ya Startimes Erick Cyprian kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuongezaka kwa chanal wakati wa kipindi hiki cha kutimiza miaka mitatu tangu ianzishwe kampuni hiyo kulia ni Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo Zuhura Hanif Picha na SUPER D |
0 maoni:
Post a Comment