Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendela(wa poli kushoto),Meneja wa wa Bia ya Safari
Lager, Oscar Shelukindo,Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa(TAPA), Fred
Mush na Katibu wa chama cha Pool Taifa , Amos Kafwinga wakiwa katika maandamano
ya ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari National Pool Championships.
Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro,Joel Bendela(wa tatu kushoto) akipigiwa makofi mara baada kufungua
rasmi fainali za mashindano ya Safari National Pool Championship 2013 Mkoani
Morogoro.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos
Kafwinga, Makamu Mwenyekiti wa chama cha Pool, Fred Mushin a Meneja wa Bia ya
Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Baadhi
ya wachezaji wa Pool kutoka mikoa 17 ikiwakilisha na vilabu 17 nchini wakiwa
katika maandamano kuelekea katika Ukumbi wa Tanzanite Morogoro wakati wa
ufinguzi wa fainali za kitaifa za Safari National Pool Championships.
Top Land- Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni Dar es Salaam
Mzamini Mkuu
wa mashindano ya Safari National Pool Championships,Meneja wa Bia ya Safari
Lager, Oscar Shelukindo(wa tatu kushoto),Mwakilishi wa TBL Morogoro,Julius
Ngaga(wanne kusho),Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Iringa, Salum Kisaku
(wa pili kushoto) na Mwamuzi wa kike pekee,Vaileth Mrema(kushoto) na baadhi ya wachezaji wakiwa katika
maandamano ya ufunguzi wa fainali za Pool Taifa Mkoani Morogoro.
Na Mwandishi
Wetu.
MKUU wa Mkoa
wa Morogoro, Joel Bendela, amewaasa chama cha Pool Taifa(TAPA), kumkumbatia
mdhamini mkuu wa mhezo wa Pool Taifa, “Safari
Lager” kupitia Kampuni kubwa nchini Tanzania Breweries(TBL).
Bendela
aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano hayo yanayoyofanyika
kitaifa Mkoani Morogoro ambapo yeye alialikwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema
Bendela, vipo vyama vya michezo vingi vinashindwa hata kufanya mashindano kwa
mwaka lakini Pool ni mwaka wa sita sasa mnafanya,vipo vyama vingi vya michezo
vinalia kwanini mpira wa miguu peke yake ndio unapata udhamini lakini Pool ni
mwaka wa sita sasa mnae mzamini na bado mnaendelea nae na baada ya hapa anaipeleka
timu ya Tifa kwenye mashindano ya Afrika ya mchezo wa Pool.
Mchezo wowote ili ukue
na kutambulika nchini na Duniani unaanza na mchezaji mwenyewe kuupenda na
kuufanya kutoka moyoni kwa kujiheshimu kwanza mwenyewe na kuuheshimu mchezo
ndipo hata jamii huudhamini(Self displine anda Tactical displine).
Alisema Bendela
yeye kama mdao na mzoefu kwenye tasnia ya michezo na mpaka sasa anashikiria
sifa kemkem ambazo hazijawahi kutolewa kwenye rekori anauzoefu wa kutosha na
maswala ya michezo,siri ya maendeleo katika michezo ni nidhamu pekee na si
vinginevyo.
Mtazamo wa
mchezo wa Pool katika jamii siku kadhaa hapo nyuma ulionekana kama mchezo wa
kihuni lakini leo mmebadilisha taswira hiyo na sasa mko kwenye mikoa 17
ikiwakilisha na vilabu 17 mkiunganisha na mchezo wa Pool mkiwa mkoani Morogoro
katika fainali za kitaifa, hongereni sana TAPA.
Mkuu wa Mkoa
pia aliipongeza TBL kupita bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mchezo
wa Pool na sasa ni mwaka wa sita ambapo aliomba waendelee kudhamini kwani
mchezo huu unaunganisha vijana wengi Tanzania kwa hapo walipofikia kwenye mikoa
17,unaepusha mambo mengi maovu ambayo wangekumbana nayo hawa vijana ni zaidi ya
vijana 300 wamekutana Mkoa wa Morogoro na kilicho wakutanisha ni mchezo wa
Pool.Endeleeni kudhmini mchezo wa Pool kwani kwa sasa michezo ni afya, michezo
ni upendo,michezo ni urafiki,michezo ni matangazo na michezo ni afya.
Bendela
aliwakaribisha wote Mkoani Morogoro na kuwaomba wawe na amani kwani Morogoro ni
shwari kabisa hewa nzuri baridi kiasi.
Nae Meneja
wa Bia ya Safarai Lager,Oscar Shelukindo alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa
kujitokeza kufungua fainali hizo na kuahidi lengo la Safari Lager na kuufanya
mchezo wa Pool kuwa mchezo namba moja kama ilivyo Safari Lager bia namba moja
Afrika hivyo wataenelea kudhamini mashindano ya Pool daima.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa, Fred Mushi alimsukuru mdhamini Safari Lager
kuendelea kuwadhamini na pia kumshukuru Mkuu wa mkoa kwa changamoto
alizozieleza za kumlinda mdhamini na kuahidi wanajitahidi kwa kadri ya uwezo
wao kuwaweka sawa vijana kuhakikisha mchezo wa Pool unakuwa chezo namba moja
nchini na Afrika kama bia ya Safari Lager.
Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga akizungumza.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo. akizungumza
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool, Fred Mushi akizungumza
Mgeni rasm,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendela akizungumza
Wadau wa habari wakiwa kazini
Mgeni rasmi akiondoka
Mgeni rasmi akiondoka
0 maoni:
Post a Comment