Malkia wa Zouk nchini Hafsa Kazinja(katikati) akiwa na Omari Mkali
(kushoto) na Abdul Salvador baada ya kukamilisha kurekodi wimbo wa 'NIMUOKEOE
NANI' katika Studio za OM Productions jijini Dar es salaam .
Omari Mkali akimuwekea mic vizuri
Na Mwandishi Wetu.
MALKIA wa
Zouk Tanzania, Hafsa Kazinja, anaibuka upya katika fani akiwa
na ingizo lake la kwanza kati ya kumi aliyoandaa kwa kuimba wimbo maarufu
wa NUTA Jazz Band uitwao “NIMUOKOE NANI” anauouleta hewani katika mahadhi
ya Zouk.
Hafsa Kazinja anasema ameamua kurudi ulingoni kwa kutoa
wimbo huo ili kumuenzi Mzee Muhidin Maalim Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani
ya muziki baada ya kufanya kazi hiyo akiwa na bendi mbalimbali tokea mwaka wa
1960.
“Nimeamua kuimba wimbo huu wa “NIMUOKOE NANI” ili
kumuenzi gwiji huyu wa muziki kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo
naibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda”, anasema Hafsa ambaye alitoka kwa
wimbo wake wa “PRESHA” aliomshirikisha Banana Zorro.
Hafsa ameandaa wimbo huo wa “NIMUOKOE NANI” katika studio za
OM Productions ya jijini Dar es salaam chini ya wanamuziki nguli, Abdul
Salvador na Omari Mkali.
“Nafurahi kwamba wimbo wa NIMUOKOE NANI nimeuimba baada ya
kupata Baraka zote toka kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe.
“Haikuwa rahisi kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya
kwenda kumuona nyumbani kwake alinifanyisha mtihani wa kuuimba wote kabla ya
kuridhika maana alisema asingefurahi kuona wimbo wake unaimbwa hovyo hovyo na
kuharibiwa radha yake”, anasema Hafsa, ambaye hivi sana anamalizia ngoma zake
zingine tisa alizotunga mwenyewe, kabla ya kuvamia anga kwa mara ingine.
Hafsa anasema katika ukimya wake amekuwa akifanya utafiti na
kujifunza kwa undani zaidi fani ya muziki, akipata mawaidha maridhawa toka kwa
wanamuziki nguli ndani nan je ya nchi wakiwemo Muhidin Maalim Gurumo, Omar
Mkali, Abdul Salvador na Lokassa ya Mbongo wa Congo aliyekutana na kufanya naye
kazi alipokuwa ziarani Marekani hivi karibuni.
Msanii huyu wa kizazi kipya anasema ataitambulisha rasmi
ngoma ya “NIMUOKOE NANI” katika tamasha la kumuenzi Mzee Gurumo lililopangwa
kufanyika OKtoba 1, 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
“Natumaini wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye
tamasha hilo name naahidi kuitendea haki ngoma ya “NIMUOKOE NANI” hivyo
wasikose kuja kujionea wenyewe jinsi sie wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya
kazi na wakubwa wetu wa kazi, anaongezea Hafsa ambaye pia anaandaa video yake
pamoja na ya ngoma zake zingine mpya.
Mkongwe Abdul Salvador, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi
wa bendi ya TANCUT ALMASI YA Iringa iliyotamba na mtindo wake wa “FIMBO
LUGODA”, anamtaja Hafsa kazinja mmoja wa wanamuziki wa kike waliojaaliwa sauti
nzuri na kipaji cha hali ya juu hapa nchini.
“Kwa kuweza kuimba wimbo wa Mzee Gurumo na kupatia
kisawasawa inadhihirisha kwamba Hafsa ni mwanamuziki aliyekomaa maana si mchezo
kuimba nyimbo ya wakongwe kwa ufasaha kama alivyofanya Hafsa.
“Na hii inadhihirisha kwamba uwezekano wa kizazi kipya na
cha zamani kufanya kazi pamoja ni mkubwa sana na sioni kwa nini isiwe hivyo”,
anasema Salvador.
PRISCA CLEMENT NDIYE MISS VIPAJI TANZANIA 2013
Mrembo
Prsica Clement, kutoka Kitongoji cha Sinza (katikati) akipunga mkono
kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Talent
kwa mwaka 2013, na kufanikiwa kupata tiketi ya kuingia hatua ya 15 bora
ya shindano la Redd's miss Tz mwaka huu.
Washiriki
wa shindano la kumtafuta mshiriki wa kuingia katika hatua ya 15 bora ya
Shindano la Redd's Miss Tanzania kwenye shindano la Redd's miss tz
Talent 2013 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi
wa hatua ya tano bora.
Mrembo
Prisca Clement ambaye ni mwakilishi kutoka Sinza na Kanda ya Kinondoni
usiku wa kuamkia leo alifanikiwa kuwabagwa warembo wenzake 26 kati ya 30
wanao wania taji la Miss Tanzania mwaka huu na kufanikiwa kuwa mrembo
wa 3 kuingia Nusu Fainali ya Mashindano hayo baada ya kutwaa taji hilo
dogo.
Shimdano hilo lilifanyika katika Hoteli ya Giraffe Ocean View ambako ndiko Kambi ya Warembo hao ilipo.
Prisca akipita jukwaani mara baada y.a kutajwa kuwa ndio mshindi
WASHIRIKI WA MISS TANZANIA WATEMBELEA KAMPUNI YA TANZANIA DISTILLERIES LIMITED 'KONYAGI'
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' David Mgwassa akizungumza na waandishi wa habari baada ya warembo wanaowania taji la Miss Tanzania kufanya zihara katika Kampuni hiyo mwishoni juzi ambayo imedhamini mashindano hayo kupitia kinywaji chake cha Zanzi .Picha na mpiga picha wetu
Baahi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakichukua chakula wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' juzi ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu
Baahi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakiwa kwenye pozi wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' juzi Konyagi ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu
Meneja masoko ya ndani na nje wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' ,Vimal Vaghmaria kushoto na meneja masoko wa ksampuni hiyo Joseph Chibhee wakigonganisha grass na Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania walipotembelea kiwandani juzi Konyagi ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu
Meneja masoko ya ndani na nje wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' ,Vimal Vaghmariakatikati akiwa katika pozi na baadi ya washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania walipotembelea kiwandani juzi konyagi ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu
Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakiwa kwenye pozi wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' juzi konyagi ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu
Baahi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakipata chakula wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi Picha na Mpiga picha wetu
NA MWANDISHI WETU
WAREMBO wanaowania taji la Miss Tanzania wametakiwa kupenda na kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries (KONYAGI) Bw. David Mgwassa wakati akiongea na Warembo 30 wanaowani taji la Miss Tanzania walipotembelea kiwanda hicho jijini Dar es salaam.
"Nyinyi ni mabalozi wazuri wa kutangaza bidhaa za humu ndani hivyo nawaomba sana mzipende na kuthamini sana bidhaa zote zinazozalishwa na viwanda vya ndani" alisema Bw. Mgwassa.
Amesema kuwa TDL kupitia kinywaji cha Zanzi imeamua kudhamini shindano la Miss Tanzania kwa kiasi cha Milioni 40 ikiwa na lengo la kutangaza kinywaji hicho na pia kuboresha shindano hilo.
Kwa mujibu wa Bw. Mgwassa shindano la Miss Tanzania ni kielelezo muhimu kwa taifa hili na kuwataka warembo hao kutangaza milima kilimanjaro na pia kuitangaza Zanzi kuwa ni bidhaa bora kwa Watanzania kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.
"Nyinyi warembo naombeni sana Zanzi iwe kwenye mawazo yenu kila siku na muitangaze Zanzi baada ya mlima kilimanjaro kwa kufanya hivyo basi uchumi wa nchiu pia utakua mzuri zaidi." alisema
Kwa upande wake meneja masoko wa TDL, Bw. Vimal Vaghmaria aliwataka warembo hao kuwa na nidhamu kubwa wanapokuwa kambini kwa lengo la kupata mrembo mwenye viwango vya juu na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
"Sisi kama TDL kupitia kinywaji cha Zanzi tumemua kudhamini shindano hili la Miss Tanzania tukiamini kuwa nyinyi ni mabalozi wazuri wa kuitangaza kinywaji hichi na kuiletea sifa Tanzania" alisema Bw. Vaghmaria.
Katika ziara hiyo warembo walipata nafasi ya kujione shughuli mbalimbali za kiwanda hicho kuanzia mwanzo wa vinywaji vinapozalishwa hadi kwenye sehemu ya mwisho ya upakiaji.
Mama Salma Kikwete awataka wanafunzi wa kike kujiepusha na Mafataki
Na Anna Nkinda – Maelezo
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanafunzi wa kike kujiepusha na
mafataki ambao watawarubuni kwa vitu mbalimbali na hatimaye kuwapatia
ujauzito na ugonjwa wa Ukimwi na hivyo kutofikia malengo waliyojiwekea
katika maisha yao.
Pia
amewataka wanafunzi wa kiume kuachana na tabia ya kuvaa suruali
milegezo na uvutaji wa sigara ambao utawasababishia kupata ugonjwa wa
kansa ya koo na mapafu.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) ameutoa wito huo hivi karibuni wakati akiongea na wanafunzi wa
shule ya Sekondari ya Msimbu iliyopo kata ya Msimbu wilaya ya
Kisarawe mkoani Pwani.
“Kama
wazazi wenu hawawasimanii kufuatilia mienendo yenu mjisimamie nyinyi
wenyewe kwa kukanyana na kutoa taarifa kwa walimu wenu pale ambapo
mtaona mwenzenu ana tabia ambazo ni kinyume na maadili ya
mwanafunzi kwa kufanya hivyo mtaepukana na tatizo la mimba za utotoni’,
alisema Mama Kikwete.
Kuhusiana
na madai ya wanafunzi hao kuwa wazazi wao wanakabiliwa na tatizo la
umaskini jambo ambalo linawafanya waweze kuingia katika vishawisi
mbalimbali Mama Kikwete alisema kuwa umaskini isiwe ni kigezo cha mtu
kufanya mambo yasiyofaa ili aweze kupata fedha jambo ambalo ni hatari
katika maisha yake.
“Ni
muhimu wazazi wakatafuta mbinu mbadala ya kuweza kukabiliana na hali hii
ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwani mtu akifanya kazi kwa bidii ni
lazima atafanikiwa na kuweza kupambana na hali ya umaskini kwani atalima
mazao na kuuza, atafanya biashara ndogondogo na kuweza kujipatia
kipato”, alisema Mama Kikwete.
Aidha
Mama Kikwete pia aliwataka wanafunzi hao kuitumia teknolojia vizuri
katika kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kujitafutia nyaraka za
kusoma “material” kwa ajili ya masomo yao na siyo tofauti kwani
teknolojia ikitumika vibaya ni rahisi mtu kuiga mambo ambayo ni tofauti
na utamaduni wake.
Akisoma
taarifa ya shule hiyo Mwalimu Mkuu Renatus Rweyemamu alisema kuwa tangu
shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 2007 hadi sasa idadi ya wasichana
waliopata ujauzito ni 34 na wahusika wameshafikishwa kwenye vyombo vya
dola na hivi sasa suala hilo linasimamiwa na watendaji wa vijiji husika.
Alizitaja
changamoto zinazoikabili shule hiyo kuwa ni wanafunzi kutembea umbali
mrefu kufuata shule jambo ambalo linasababisha kuingia darasani wakiwa
wamechoka pia wasichana wanakutana na vishawishi vingi wakiwa njiani,
hosteli moja haitoshi kwa kuwa inauwezo wa kuchukua wanafunzi 48 pia haina vitanda wala magodoro ya kulalia.
Mwalimu Rweyemamu
alisema, “Changamoto nyingine ni wazazi kutofuatilia kwa ukaribu
mienendo ya watoto wao pia kutokutoa ushirikiano wakati wa kuwafuatilia
wahusika waliowapatia ujauzito watoto wao”.
Aliiitaja
mikakati waliyojiwekea kuwa ni kufanya mikutano na wazazi ili kuwapa
ushauri jinsi gani wanaweza kufuatilia mienendo ya watoto wao na
kutafuta wafadhili watakaowasaidia kujenga Hosteli ikiwa ni pamoja na
kununua vitanda, magodoro na kuweka umeme jua.
“Pamoja
na majukumu mengi yanayokukabili ombi letu kubwa kwako kwa sasa ni
tunaomba kama itawezekana utununulie vitanda na magodoro kwa Hosteli
yetu”, alisema Rweyemamu.
Shule
ya Sekondari ya Msimbu ni shule ya kata ambayo inajumla ya wanafunzi
463 wasichana wakiwa ni 250 na wavulana 213 ambao wanatoka katika vijiji
sita vilivyopo katika kata ya Msimbu.
PICHA ZAIDI YA MPAMBANO WA FLOYD MAYWETHER NA CANELO ALVAREZ
Bondia floyd mayweather kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na canelo alvarez wakati wa mpambano wao mayweather alishinda kwa point
MATOKEO KAMILI YA MPAMBANO WA floyd mayweather vs canelo alvarez Judges Dave Moretti (116-112) and Craig Metcalfe (117-111) scored the fight in favor of Mayweather, while C.J. Ross scored it a 114-114 draw.
MPAMBANO UKIENDELEA
Mapacha Watatu Band FC, Mashujaa Band FC hakuna mbabe
Kikosi cha Mapacha Watatu Band FC
Kikosi cha Mashujaa Band FC
MECHI
iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Mapacha Watatu FC na
Mashujaa Band FC imeisha vizuri huku timu zote mbili zikifungana bao
1-1, katika mchezo uliochezwa jana katika Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mchezo
huo uliondaliwa na kundi la Bongo Dansi linalopatikana kataika mtandao
wa kijamii wa facebook kwa nia ya kuletaa ushirikiano na undugu kwa
wanamuziki.
Ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka iliyoacha simulizi kubwa kwa wote walioishuhudia. Hadi Mapumziko, Mapacha Watatu walikuwa mbele kwa kwa bao lililofungwa na Hija Ugando dakika ya 19.
Mfungaji
alifunga kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na Hamis Dacota aliyeichambua
ngome ya Mashujaa kabla ya kutoa pande kwa mchezaji mwalikwa Mathew
Kiongozi ambaye naye bila hiyana alimsogezea Hajji aliyeujaza mpira
wavuni.
Wachezaji
wa Mapacha wakiongozwa na Jose Mara, Khalid Chokoraa, Kasongo, Dacota ,
Dulla Ngoma na wengineo, waliendelea kulisakama lango la Mashujaa kwa
muda wote wa kipindi cha kwanza.
Lakini
Upepo ulibadilika kipindi cha pili ambapo Chaz Baba, Abdul Tall, Jado
FFU na wengineo walianza kuumiliki mpira na na kuwafunika Mapacha
Watatu.
Zikiwa zimesalia dakika 3 mpira
kumalizika, Mashujaa walisawazisha kwa bao lililofungwa na Hamis Tanya,
ikiwa ni hatua nzuri ya maendeleo ya kundi hilo la Bongo Dansi,
lililoanzishwa na kuongozwa na wadau wa muziki, akiwamo Said Mdoe,
Mathew Kawogo ama Mathew Kiongozi, Engi Muro Mwanamachame, William
Kaijage na Abdulfareed Hussein, Deo Mutta Mwanatanga na Khamis Dacota.
0 maoni:
Post a Comment