MISS
Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji
la Redd’s Miss Tanzania 2013 usiku wa Septemba 21, Ndani ya Ukumbi wa Mlimani
City na kuwashinda warembo wenzake 29.
Na Father
Kidevu Blog
HATIMAYE
kitendawili cha nani atanyakua taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 kimeteguliwa
usiku huu na mrembo Happiness Watimanywa kutoka Mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati
kufanikiwa kutawazwa Mshindi wa taji hilo na kuwashinda warembo wengine 29
waiokuwa wakiwania taji hilo.
Nyota ya
Happiness ilionekana dhahiri kung’aa vyema katika fainali hizo mwaka huu tangu
pale alipofanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa mrembo
wa kwanza kuingia nusu fainali.
Wakati
Happiness akinyakua Taji hilo pamoja na zawadi ya Gari na kitita cha shilingi
Milioni 8 nafasi ya pili ilikwenda kwa mrembo Latifa Mohamed kutoka Kitongoji
cha Kigamboni na Kanda ya Temeke na nafasi ya Tatu ikienda kwa Miss Tanzania
Sports Woman, Clara Bayo.
Pamoja nao
warembo wengine walio ingia hatua hiyo ya tano bora ni Lucy Tomeka na Elizabeth
Prety.
Hii
ndio tano bora ya Redd's Miss Tanzania 2013. Je nani hapa ataondoka na
taji, gari na kitita cha Milio ni 8? Warembo hao kutoka kushoto ni
Happiness Watimanywa (Miss Photogenic), Elizabeth Pretty, Clara Bayo
(Miss Sports Women), Lucy Tomeka na Latifa Mohamed.
Fainali
za Miss Tanzania 2013 ndio zinaendelea usiku huu ndani ya Mlimani City
jijini Dar es Salaam. Gari ndo hilo hapo Je nani ataingia ndani na
kuliendesha? Tusubiri Majaji. Hadi sasa Top 5 ndo ishatajwa.
AL SHABAAB WATHIBITISHA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA KIGAIDI NAIROBI
Baadhi ya majeruhi katika shambulio la kigaidi jijini Nairobi.
-Wadai Kenya ilipuuza onyo lao
-Wasema ni kulipiza kisasi kwa Kenya kijihusisha katika vita ya Somalia
-Watu zaidi ya 30 wadaiwa kupoteza maisha wengine wakijeruhiwa
KUNDI la Alshabaab, limethibitisha kuhusika na shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya.
Alshabaab kupitia kwa afisa wake mmoja, imethibisha hilo na kueleza kuwa shambulio lilikuwa na kulipiza kisasi baada ya Kenya kujihusisha na vita ya Somalia.
Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.
Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi.
Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo alifariki kutokana na majeraha yake. Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

Al shabaab wadai kuhusika na shambulio la kigaidi jijini Nairobi, 30 wahofiwa kuwawa na ziaid ya 50 wamejeruhiwa
Na Kenneth Kinonko wa Globu ya Jamii, Nairobi
Magaidi wa kundi la Al Shabaab limesema kuwa linahusika na shambulio katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi mchana wa Jumamosi Septemba 21, 2013 ambalo limeacha zaidi ya watu 30 kuuwawa.
Magaidi wa kundi la Al Shabaab limesema kuwa linahusika na shambulio katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi mchana wa Jumamosi Septemba 21, 2013 ambalo limeacha zaidi ya watu 30 kuuwawa.
Kupitia ujumbe wao katika mtandao
wa twitter, kundi hilo limesema shambulio hilo ni ujumbe kwa Serikali ya
Kenya kuitaka iondoe majeshi yake yote kutoka Somalia. Kundi hilo pia
limedai kuwa limeua watu zaidi ya idadi inayotajwa na vyombo vya usalama
vya Kenya.
Hata hivyo, Waziri wa mambo ya
Ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku amesema serikali bado haijabaini ni nani
wamehusika na shambulio hilo.
Wakati huo huo idadi ya watu wanaosadikiwa kuuwawa imetajwa kuwa ni 30 na zaidi ya 50 wamejeruhiwa
Askari kanzu na mtutu wake mkononi akishikilia tumbo baada ya kujeruhiwa
Wateja wakihaha ndani ya duka hilo
Askari kanzu wakitafuta magaidi chumbha hadi chumba
Watu wakitembea kwa magoti na mikono mbele ya mwenzao mmoja ambaye inaonesha amedhakufa
Askari
kanzu na mtutu wake mkononi akimuokoa mtoto na mwanamke kutoka eneo la
tukio katika picha hii nadra ambayo inaeleza kila kitu. |
0 maoni:
Post a Comment