Naibu Waziri
wa Utamaduni,Vijana na Michezo, Amos Makala(wa tatu kulia) akimkabidhi kikombe
nahodha wa klabu ya Topland ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni,Omari Akida mara
baada ya kuibuka mabi ngwa katika fainali za kitaifa za mashindano ya Safari
National Pool yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.
Mchezaji Bora wa mwaka 2013,Godfrey Swai kutoka klabu ya Top Land ya
mkoa wa kimichezo wa Kinondoniakionyesha zawadi yake mara baada ya
kukabidhiwa
Nahodha wa klabu ya Top Land akionyesha kitita cha shilingi 5,000,000/=
Picha ya Pamoja.
Na Mwandishi
Wetu.Morogoro.
KLABU ya Top
Land kutoka mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wameibuka
mabingwa katika fainali za kitaifa za mashindano ya Safari Pool 2013,
yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.
Top land
walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga klabu ya Mpo Afrika ya Temeke 13-10 na hivyo
kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 5,000,000/=, Kikombe na medali za Dhahabu kwa
kila mchezaji.
Mshindi wa
pili katika fainali hizo ni klabu ya Mpo
Afrika ambayo ilizawadiwa fedha taslimu shilingi 2,500,,00/= na Medali za Fedha
kwa kila mchezaji.
Mshindi wa
tatu ni klabu ya Supersport kutoka mkoa
wa Manyala ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1,250,000/= na medali za
shaba na mshindi wan ne ni klabu ya Mashujaa kutoka mkoa wa kimichezo wa Ilala
ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1,000,000/=
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume(singles), mchezaji Festo Yohana kutoka klabu ya
Mashujaa ya mkoa wa kimichezo wa Ilala alitwaa ubingwa wa Taifa kwa kumfunga Mussa
Mkwega kutoka Morogoro 5-1 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi
700,000/=,Kikombe na medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili ulichukuliwa na
Mussa Mkwega ambaye alijinyakulia fedha taslimu shilingi 350,000/= na
medali ya Fedha.
Mshindi wa
tatu ni Mohamed Idd kutoka klabu ya Atlantic ya mkoani Dodoma ambaye
alizawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/= na medali ya shaba ambapo mshindi wa
nne ni Ernest John kutoka Tabora ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi
150,000/=.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanawake(Singles), mchezaji Rose Deus kutoka mkoa wa
Morogoro alitwaa ubingwa wa kitaifa kwa kumfunga Cecilia Kileo kutoka Ilala 5-4
na hivyo Rose kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/= Kikombe na medali ya
Dhahabu ambapo Cecilia alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu
shilingi 200,000/=na medali ya Fedha.
Nafasi ya
tatu ilichukuliwa na mchezaji Merry Gumbu kutoka Arusha ambaye alizawadiwa
fedha taslimu shilingi 150,000/= na medali ya shaba na nafasi ya nne ilichukuliwa
na Judith Machafuko kutoka mkoa wa Kinondoni ambaye alizawadiwa fedha taslimu
shilingi 100,000/=.
Fainali hizo
za kitaifa zilihudhuliwa na Naibu Waziri wa Utamaduni,Vijana na Michezo, Amos
Makala ambaye alikipongeza chama cha
Pool Taifa(TAPA) kwa kuufikisha mchezo hapo ulipo ambapo mpaka sasa umesambaa
katika mikoa 17 ambayo ilishiriki mashindano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano
wa kutosha kama serikali kwa kuutambua na kutoa mchaada watakapohitaji.
Makala pia
aliipongeza TBL kupitia Bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mchezo wa
Pool kwa mwaka wa sita sasa na kuwaomba waendelee kudhamini kwa miaka
ijayo.Lakini pia alimpongeza Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo kwa
Brand yake ya Safari kuwa bia namba moja Afrika na kumuomba aendelee kudhamini
Pool ikamate namba moja katika mashindano ya Pool ya Afrika yanayotarajiwa
kufanyika Malawi hivi karibuni.
Nae Meneja
wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo alikipongeza chama cha Pool kwa
kumaliza fainali salama na kuahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo, lakini
pia aliwapongeza Mkoa wa Pwani ambao mwaka huu ni mra yao ya kwanza kushiriki
fainali hizo.
0 maoni:
Post a Comment