Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Sunday, November 3, 2013

MASHINDANO YA MBIO ZA MITUMBWI YA BALIMI MKOA KAGERA YAFANA.


Mashindano ya mbio za Mitumbwi mkoa wa Kagera  ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager zimefanyika leo katika fukwe za Spice Hotel mjini Bukoba, washindi kupatikana na kukabidhiwa vitita vya zawadi. Ambapo Fainali ya kanda yatafanyika Jijini Mwanza mwezi ujao tarehe 7 novemba, 2013.
Huduma ya kutoa vifaa kwa ajili ya kujikinga ikiendelea kabla ya mashindano kuanza
Vijana kazi wakianza kujiandaa kabla ya mtanange huo mkali wa kusaka washindi wa kuwakilisha kwenye  huko jijini Mwanza tarehe 7/12/2013
Mitumbwi ikishakaguliwa na hapa ni kuingia tu kuanza mashindano rasmi
Katika kuchukua matukio ya bukobasports.com ilibidi na mimi nivae kama mwanamshindano ili niweze kuchukua picha vizuri tayari kufukuzana na mashindano hayo makubwa ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager.
Kazi imeanza...
Ilichukua muda wa dakika kama 40 kwenda mpaka mwisho na kugeuza kurudi walipoanzia
Mgeni rasmi RPC Kagera(katikati) ACP-Philip Kalangi (katikati), kulia ni Mwenyekiti Makasia mkoa wa Kagera Bw. Faraji Mugaye na (kushoto) ni Mwenyekiti Makasia Taifa Bw. Richard Mgabo
Mashindano yakiendelea pia kulikuwa na burudani safi zikiendelea hawa ni Vijana wa hapa Bukoba wanajulikana kwa jina la wasafi..
Kila mtumbwi ulitaka ushinde na kunyakua kitita


Burudani ikiendelea..




Wanawake nao walikuwepo kwenye mtanange huo mkali wao raundi yao walikuuwa na mitumbwi 12
Sehemu ya mwishoni lazima upite nje ya bendela hiyo nyeupe na kutafuta nyingine na kugeuka ulipotoka!
Wanawake wakiwajibika kutaka kupata ushindi hapa




Wanawake hao wakipiga Kasia kwa kwenda mbele!!

Wazungu nao walikuwepo kushuhudia mitanange hiyo

0 maoni:

Post a Comment