Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Wednesday, December 18, 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA MARA BAADA YA NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE ILIVYOPATA DHORUBA KIDOGO KATIKA UWANJA MDOGO WA NDEGE WA ARUSHA

Muonekano wa ndege ya Ethiopian Airline baada ya kutua kwa dharura.
Watu 200 waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya Ethiopian Airline wanusurika kufa baada ya ndege kupitiliza hadi nje ya uwanja mdogo wa ndege wa Arusha baada ya kutua kwa dharura.


Ndege aina ya Boeing 767 inayosadikiwa kuwa ni ya Shirika la Ndege la Ethiopia imetua kwa dharura majira ya saa tisa alasiri katika kiwanja cha kurushia ndege ndogo cha Arusha badala ya kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, KIA.
Abiria zaidi ya mia mbili waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamenusurika kifo, wanasubiri msaada ngazi waweze kushushwa.Picha Kwa Hisani ya DJ SEK BLOG

HUYU HAPA MWANDISHI WA HABARI MUONJAJI BORA WA BIA MWANZA 2013-2014.

Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la wanahabari la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Willy Mlinda, katika hafla fupi iliyofanyika jana katika kiwanda cha bia kilichopo Ilemela jijini Mwanza, zoezi ambalo hufanyika kila mwaka likiwa na nia ya kudumisha mahusiano baina ya kiwanda hicho na wanahabari.
Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa shindano la wanahabari la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Moses Mathew wa Mwananchi Communication, katika hafla fupi iliyofanyika jana katika kiwanda cha bia kilichopo Ilemela jijini Mwanza. 
Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu wa shindano la wanahabari la Beer Tasting Competition (Muonjaji Bora wa Bia) Charles Masamba, katika hafla fupi iliyofanyika jana katika kiwanda cha bia kilichopo Ilemela jijini Mwanza.
Awali kabla ya shindano la uonjaji bia,  Mpishi mkuu wa Kampuni ya Bia TBL tawi la Mwanza Oscar Kilasi alitoa somo kwa waandishi hao juu ya kuzibaini tofauti za bia kupitia ladha, rangi, harufu na viwango vya alcohol.
Naye Afisa Ubora wa bia za TBL tawi la Mwanza Jeremiah Kamambi alitoa somo Wajibu wa Muuzaji na Mnywaji wa bia likiwemo suala la kuzingatia afya na umri sahihi kwa watumiaji kileo.
Afisa Mahusiano wa TBL Tanzania Doris Malulu akizungumza na wanahabari dhamira ya Kampuni yake kuliendeleza shindano hilo kwa kuliboresha miaka baada ya miaka ikiwa ni pamoja na ndoto ya kulifanya shindano hilo kuwa la kitaifa zaidi kwa wadau wa habari toka mikoa mbalimbali nchini kushindanishwa.
Hapa kuna inshu ilijitokeza ya kusisimua......
Mwandishi George Nteminyanda akijaribu kuzibaini na kuziainisha aina za bia toka kwenye glasi sita zenye bia tofauti katika shindano la Beer Tasting Competition lililofanyika katika kiwanda cha TBL Mwanza.
Mwandishi Moses Mathew akijaribu kuzibaini na kuziainisha kwa kuonja na kutizama rangi aina za bia toka kwenye glasi sita zenye bia tofauti katika shindano la Beer Tasting Competition lililofanyika katika kiwanda cha TBL Mwanza.
Mwandishi Asia Mohamed akionja moja ya glass sita ili kubaini aina ya bia kwenye shindano hilo.
Toka chumba cha Ushindani TBL Mwanza.
Afisa Mahusiano wa kampuni ya bia TBL Tanzania Doris Malulu akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Mabere Makubi wa ITV (kushoto) na Charles Masamba jinsi hatua za uzalishaji zinavyofanyika ndani ya kiwanda cha TBL Mwanza.
Hiki ndicho kinachofanyika.
Uzalishaji ukiendelea kitengo cha uwekaji nembo za bia.
Usafishaji chupa.
Hatua kwa hatua..
Afisa Mahusiano wa kampuni ya bia TBL Tanzania Doris Malulu akitoa ufafanuzi kwa mwandishi wa habari Sitta Tuma.
Kinachotolewa ufafanuzi.
Taswira ya utalii kiwandani TBL Mwanza.
Safari ya utalii kiwandani katika eneo la uzalishaji ilikoma suala lililofuata likawa ni ukabidhi zawadi kwa washindi ambapo picha za washindi unaziona juu kabisa.
Zawadi kwa Philbert Kabago.
Zawadi kwa Mkurugenzi wa Gazeti la Baruti .
Zawadi kwa idara ya usafiri waandishi.
Albert G. Sengo.
Hussein Mtanda.
Sitta Tuma na kwa engo kulia ni uchokozi wa Nteminyanda.
Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akizungumza na waadnishi wa habari kiwandi eneo la Ilemela jijini Mwanza juu ya hatua mbalimbali za maboresho ya kiwanda na taratibu za kumfikia mteja kwa wakati.
Meneja wa Bia Tawi la Mwanza (TBL) Richmond Rymond akizungumza na waadnishi wa habari kiwandi eneo la Ilemela jijini Mwanza juu ya hatua mbalimbali za maboresho ya kiwanda na taratibu za kumfikia mteja kwa wakati.
Kutoka kushoto Mbaya, Erick (Afisa Matukio TBL Mwanza), Kabago na  Afisa Mahusiano wa TBL Tanzania Doris Malulu.
Picha ya pamoja ya wanahabari washiriki wa shindano la Beer Tasting Competition 2013-2014 lililofanyika katika kiwanda cha bia TBL Mwanza. 


TANZANIA DISTILLERIES LIMITED(TDL) YAZINDUA PROMOSHENI YASHINDANO LA KUMSAKA MSHINDI ATAKAE PATA FURSA YA KWENDA KUTEMBELEA SHAMBA KUTENGENEZA KINYWAJI CHA AMARULA NCHINI AFRIKA KUSINI LIJULIKANALO KAMA “AMARULA PAN AFRICAPROMOTION”.


Meneja wa kinywaji cha Amarula kutoka Kampuni ya Konyagi Tanzania, Diana Baliagati, akizungumza na waandishi wa habaari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya kinywaji hicho Mlimani City Dar es Salaam.Mshindi wa promosheni hiyo atapata fursa ya kwenda Afrika kusini na rafiki yake kwenda kushuhuduia shamba na utengenezaji wa kinywaji hicho.


Meneja wa kinywaji cha Amarula kutoka Kampuni ya Konyagi Tanzania, Diana Baliagati(kulia), akizungumza na waandishi wa habaari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya kinywaji hicho Mlimani City Dar es Salaam. Mshindi wa promosheni hiyo atapata fursa ya kwenda Afrika kusini na rafiki yake kwenda kushuhuduia shamba na utengenezaji wa kinywaji hicho.

KAMPUNI ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL) leo imetangaza promosheni ya shindano la kumsaka mshindi wa anayetumia kinywaji cha Amarula, kinacho tengenezwa nchini Afrika Kusini na kusambazwa na TDL nchini maarufu kama nyumba ya Konyagi katika promosheni iliyozinduliwa leo Shoprite Mlimani City jijini Dar es Salam ijulikanayo kama  Amarula Pan Africa Promotion”.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Bidhaa wa TDL, Diana Baliagati alisema shindano hili la kumsaka mtumiaji wa Amarula litaanza rasmi Desemba 16,2013 hadi Januari 14, 2014.
Diana alisema lengo hasa ikiwa ni kuwapa fursa wanywaji wa Amarula kwenda kutembelea nchi ya Afrika Kusini na kushuhudua shamba la Amarula na kujionea matunda ambayo hutumika kutengenezea kinywaji cha Amarula.
Mshindi katika shindano hili,atapata tiketi moja itakayomuwezesha kusafari na mwenzake kwa ajili ya kwenda kushuhudia shamba la AMARULA,nchini Afrika Kusini na kufikia katika Hoteli ya nyota tano(5Star), alisema Diana.
Meneja bidhaa wa TDL, Diana Baliagati alisema, ili kupata nafasi ya kujishindia tiketi,mshiriki anapashwa kujaza kuponi zilizo katika shingo ya chupa kubwa za Amarula zinazouzwa katika maduka makubwa yote ya Shoprite husika.Chupa hizo za shindano la Amarula Pan Africa Promotion zitakuwa zikipatika kwenye maduka ya Shoprite tu.
Mshindi wa Amarula Pan Africa Promotion atapatikana  kupitia droo itakayofanyika Januari 14,2014, na safari itakuwa mwezi Februari.Mshindi atapewa taarifa zote zinazohusika na safari  hiyo mara baada ya droo kufanyika.
 

BONDIA FRANSICI MIYEYUSHO AJIFUA KWA AJILI YA KUMTWANGA DAVID CHALANGA WA KENYA DESEMBA 31



Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akielekezwa jinsi ya kutupa makonde kwa mpangilio na Doi Miyeyusho wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika GYM ya lazima ukae iliyopo kinondoni Dar es salaam Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake wa kimataifa wa kufunga mwaka na David Chalanga wa Kenya mpambano utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Fransic Miyeyusho kushoto akielekezwa jinsi ya kutupa makonde kwa mpangilio na Doi Miyeyusho wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika GYM ya lazima ukae iliyopo kinondoni Dar es salaam Miyeyusho anajiandaa na mpambano wake wa kimataifa wa kufunga mwaka na David Chalanga wa Kenya mpambano utakaofanyika Desemba 31 katika ukumbi wa Msasani klabu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

0 maoni:

Post a Comment