Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kaghasheki amejiuzulu wadhifa
wake baada ya mjadala mkali wa Bungeni mjini Dodoma hivi sasa. Habari
zaidi kwa kirefu zitakuja baadaye. Hii inatokana na Operesheni Tokomeza
iliyolenga kuondoa ujangili uliokithiri nchini.
Tangu
kuanza kwa operesheni hiyo, kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka
kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa
wakiiendesha yakiwamo ya watu kujeruhiwa, kuchomewa nyumba, mifugo
kuuawa, kupigwa,kubakwa na uporaji.
Operesheni
hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa pamoja na askari wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (Tanapa).
Operesheni
hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga bungeni na watunga sheria hao
kuweka kando tofauti zao za kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki
na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Mathayo David Mathayo
wawajibike.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo David, naye pia amegoma kujiuzulu baada ya kutoa utetezi wake mrefu. Amedai pia kuwa ameonewa.
Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ametaka uthibitisho usio na shaka kwa
waliohusika wote na taasisi zao kuchunguzwa kiundani ili hatua stahiki
zichukuliwe. Kuendelea kulinda rasilimali na hifadhi za Taifa ameutaja
kuwa ni muhimu. Pia amesema ameongea na Waziri mmoja mmoja kuwa ni
busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Amebainisha kuwa hata baada ya
kuongea na Rais. mkuu wa nchi ameridhia tume iundwe na kila aliyehusika
awajibike.
Amesema Rais ameshauri kutengua uteuzi wa mawaziri wote wanne ( Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Wazir wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt David Mathayo, na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki) kama ambavyo wabunge walivyopendekeza.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe James Lembeli
(pichani juu) amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na matokeo ya ripoti
ya kamati iliyosababisha hayo yote, na kwamba maelezo ya taarifa ya
kamati kimsingi yote yamekubalika.
Kuhusu kumhusisha Dkt Mathayo ni kuwa Rais alishatoa maagizo tisa miongoni likiwepo swala la kushughulikia wafugaji wanaohamahama. Amesema pia Rais aliagiza pia kuwa wafugai wawe wa kisasa, pia kutafuta missing link ya mifugo isipotee na pia kutafuta masoko nje ya nchi, ambapo amesema mengi hayajatekelezwa. Ameweka bayana kuwa chimbuko kubwa ni Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, na kwamba Waziri hakuwa anapewa taarifa za mara kwa mara. Ameomba kipengele kiongezwe kuwa Katibu mkuu na watendaji wake wakuu waliohusika kuandaa Mpango kazi wa 'Operesheni Tokomeza' wawajibishwe. Amesema rushwa iliyoko ndani ya wizara ya Maliasili na Utalii inatisha. Spika amuomba Mwanasheria mkuu kutumia kifungu kuongeza muda. Naye ameomba kuundwa tume ya kisheria ya mahakama. Spika Mhe. Anne Msekwa ameahirisha Bunge (saa tatu na dakika nne usiku huu) hadi saa tatu kesho asubuhi.
SOURCE MICHUZI BLOG.
Juu ni Dkt Emmanuel Nchimbi na chini ni Mhe Shamsa Vuai Nahodha
|
0 maoni:
Post a Comment