Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Saturday, June 25, 2011

MWANAMUZIKI KUTOKA JAMAIKA AFUNIKA VIBAYA SANA TAMASHA LA ZIFF ZANZIBAR

Mwanamuziki kutoka Jamaika, Shagyy akiimba jukwaani wakati wa tamasha la Filamu la Nchi za Majahazi Zanzibar

Na Andrew Chale, Zanzibar
MWANAMUZIKI wa kimataifa wa ragga na mshindi wa tuzo za Grammy 2011, Orville Richard   ‘Shaggy’  usiku wa kuamkia leo aliweza kupia shoo kali na ya ndani ya Ngome kongwe kwa zaidi ya masaa manne na kuvunja rekodi ya pekee kwa kupiga shoo ndefu kwa afrika.Shaggy alipiga shoo hiyo maalum kwenye tamasha la filamu za nchi za majahazi maalufu kama (Zanzibar International Film Festival-ZIFF) ziilizofanyika ndani ya Ngome kongwe na kufurika mamia wa mashabiki kumshuhudia mjamaika huyo anayeishi marekani. Katika shoo hiyo ambayo ilisindikizwa na kundi la dansa la nyumba ya vipaji la THT, pamoja na wasanii wa Zanzibar, akiwemo Baby J na Sultan King, Shaggy alipanda jukwaani majira ya saa sita kamili usiku ambapo umati wa mashabiki ulifurika kwa shanngwe na nderemo kubwa kutokana na kutaka kumuona ..kama kawaida ya Shaggy ambaye mara zote amekuwa mwenye mizaha mingi na utani alianza kuimba baadhi ya nyimbo zake zinazotamba Duniani kote  kwa hali hiyo umati huo uliendelea kupiga kelele za  shangwe na Shaggy alimua kusimamisha mziki na kutoa shukrani zake."Mimi ni Mjamaika nawapenda Zanzibar wote tamaduni zangu zinafanana na zenu, Zanzibar ni kisiwa cha amani hivyo nitatumia nafasi ya pekee na ya kihistoria leo hii na dunia itajua" alisema Shaggy na kisha aliomba apigwe picha maalum akiwashukuru wa zanzibar kwa kumuunga mkono ambapo alisimama mbele ya jukwaa na kuwageuzia mgongo na kupiga picha mbele ya umati.Shaggy baada ya kumaliza zoezi hilo laiweza kupiga shoo zaidi ya masaa matatu bila ya kusimama ikiwemo nyimbo zake za Boombastic, Angel,  Sex lady, Feel  the Rush na nyimbo nyingi zilizo kuwa ndani ya Albam yake...Hata hivyo baada ya majira ya saa nane na nusu Shaggy alipomaliza nyimbo zake Mc wa shoo hiyo baada ya kupanda jukwaani na kuwashukurub wananchi kwa kujitokeza ...ghala Shaggy akapanda tena jukwaani na kuwaambia wa mashabiki kuwa atapiga muziki mpaka asubuhi kwa hiyo, mashabiki hao walirudi ukumbini hapo na Shaggy aliendelea na muziki mpaka saa 10 usiku ndipo alipomaliza rasmi na kuwashukuru huku akiongea moja ya maneno ya kiswahili ..'Mambo' , vipi na poa ..Awali Shaggy alitua na boti maalum visiwani hapa majira ya saa  10 jioni na kisha kuongea na waandishi wa habari ndani ya Hoteli ya Zanzibar Beach Reasort, Shaggy aliweza kuisifia Zanzibar na kuhahidi kuweza kufika mara kwa mara kwani mazingira ya kisiwa hicho kinafnana na nchi yake ya Jamaika."Naipenda, Zanzibar si mara ya kwanza kuja hapa Tanzania, maisha ya hapa na mazingira nib kama nyumba, hivyo ni fursa ya pekee kwangu kutoacha kuja nitakuja mala kwa mara..naipenda Zanzibar nawapenda wazanzibar" alisema Shaggy.Kwa mara ya kwanza, tamasha hilo limedhaminiwa na  Kampuni ya Bia ya Serengeti, kupitia kinywaji chake cha Tusker Malt, huku wengine ni  Prime Time promotion, Coconut FM, Azam Marine Co ltd, TTB, Common Wealth Foundation, Coca-Cola, GIZ (TZ), na Ujerumani, Smole, Movenpick, Kituo cha Utamaduni cha Ufarans



0 maoni:

Post a Comment