Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Thursday, June 23, 2011

EXTRA BONGO WAACHA HISTORIA MIKOA YA KUSINI


Na Michael Machellah

BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo imeacha historia ya Pekee kwenye Mikoa ya Kusini wakati wa ziara ya siku tatu katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Kijijini Utete.

Akizungumza na Mtandao wa Extra Bongo, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Chocky amesema shoo zote zilikwenda vizuri watu walijaa sana hata kuonekana kumbi zilizokuwa zimeandaliwa kuwa ndogo.

Chocky alisema, Mkoani Lindi watu walijaa sana hivyo kuwataka wapige tena siku inayofuata lakini haikuwezekana kwani ratiba ilibana walipaswa kupiga Mtwara,ambapo vivyo hivyo Mwara napo watu walijaa sana hivyo wakazi wa Kusini wakaomba ipangwa ratiba nyingine ya kutembelea mikoa hiyo.

Bendi ya Extra Bongo kwa sasa imesharejea na leo wanatarajia kufanya onyesho kwenye Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo wanawake ni bureeeeee.

Chocky amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza kwenye onyesho hilo wajionee mambo mapya ya Bendi yao na style mpya za uchezaji.

0 maoni:

Post a Comment