Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Tuesday, July 5, 2011

MASHINDANO YA POOL SAFARI LAGER DAR NI PATASHIKA NGUO KUCHANIKA


Na Michael Machellah

MASHINDANO ya Pool Safari Lager yaliyoanza jana katika Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam kundi A:Shoko na Mkwajuni wakati kundi B:Topland na 4Ways zaanza vyema kwa ushindi wa kishindo.

Mechi za ufunguzi wa mashindano hayo zilianza jana kwenye Klabu ya Mwanese Mabibo jijini Dar es Salaam ambapo ambapo kundi A,timu ya Shoko ilianza kucheza na Meeda ambapo ilibuka na ushindi wa pointi 15-10, na timu ya Mkwajuni ilianza na Jaba ambapo Mkwajuni ilishinda 15-10.Kundi B,Topland ilianza na Bahama Mama ambapo Top Landa ilishinda 17-8 na 4ways ilianza na Madrid na 4ways ikashinda 14-11.

Mashindano hayo yalifungulia rasmi mnamo saa nne aasubuhi na Katibu Mkuu wa chama cha Pool Mkoa wa Kinondoni, Zaholo Ligalu kwa kuwataka wachezaji wawe na utulivu kwani kati yao ndipo itapoundwa timu ya Mkoa.

Timu zinazoshiriki mashindano ya Mkoa wa Kinondoni ziko kumi ambazo zimegawanywa katika makundi mawili ambapo kundi A ni Jaba,Shoko,Meeda,Mkwajuni na Ubungo ambapo kundi B, ni Topland,Bahama Mama,4Ways,Madrid na Mlalakuwa.

0 maoni:

Post a Comment