
Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza na moja ya wapenzi na shabiki wa Bendi hiyo wakati wa onyesho kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky akiimba sambamba na Mpiga Bass wake, Hoseah Mgoati

Kiongozi wa wacheza shoo, Super Nyamwela akipiga tumba wakati wa onyesho hilo.

Mpiga Bass, Hosea Mgoati sambamba na Rapa, Saulo Fagason wakitunzwa na moja ya wapenzi wa Bendi hiyo

Fagasoni akirap sambamba na wapenzi

Aha........Hosea Bass....

Ally Chocky akiimba sambamba na wapenzi na mashabiki

Chockyyyyyyyyyyyyy.......

Hoseah Bass akikata kiuno sambamba na sabiki..

Ah....... Fagasoniiiiii......

Hapo sasa.......

Mcheza shoo, Angel asiyependa masihara kazini akiwafanya vitu vyake kuwapa burudani wapenzi na mashabiki

Mpiga Drum,Martine Kibosho akifanya vitu vyake

Fagasoni akiimba sambamba na wacheza shoo

Hoseah Bass akipiga Gitaa sambamba na Mpuga Drum Martine Kibosho

Mwimbaji mahili, Athanas Motanabe akipiga Tumba
Na Michael Machellah
BENDI ya Muziki wa Dansi ya Extra Bongo Next Level wanatarajia kuwasha moto ndani ya Meeda katika sherehe za Idd Mosi kwa wapenzi na mashabiki wa Sinza Jijini Dar es Salaam
Akizungumza na Mtandao wa Extra Bongo Mkurugenzi wa Bendi hiyo, Ally Chocky amesema baada ya kuzikonga nyoyo za wakazi wa Sinza Idd pili watahamia Gongo la Mboto katika Ukumbi wa Wenge ambako wanatarajia kufanya kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa wapenzi na mashabiki wa Muziki wa Dansi.
Alisema Choki wakiwa katika maandalizi hayo pia Bendi iko msituni katika kurekodi Video ikiandaa albam amabyo mpaka sasa bado hawaipatia jina.
‘Wapenzi na mashabiki wa Bendi ya Exta Bongo kaeni mkao wa kupata burudani safi na nzuri ambayo hamjawahi kuipata katika kipindi chote kuanzia sasa kutoka kwa vijana mahili wa Kitanzania ambao wanaweza kujisimamia wenyewe na kujiongoza wenyewe’ alisema Chocky.
0 maoni:
Post a Comment