Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Friday, December 23, 2011

EXTRA BONGO KUWASHA MOTO MKESHA WA X-MASS NDANI YA MEEDA

Na Michael Machellah
MKURUGENZI wa Bendi ya Extra Bongo,Ally Chocky aahidi kufatoa burudani ya pekee katika Mkesha wa Chrismas,jumamosi katika Ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Chocky amesema katika shoo hiyo patakuwa na ushindani wa pekee kati ya wanamuziki na wacheza shoo ambapo Mkurugenzi mwenyewe,Ally Chocky atapanda jukwaani kuchuana na Mwalimu wa walimu,Banza Stone kwa kutoa shoo na baaada ya hapo watahamia kwa wacheza shoo wa kike ambapo Mkongwe wa Dance, Aisha Mbegu atachuana na Otilia Boniphace (Kandoro).


Murugenzi alisema, katika onyesho hilo la Mkesha wa Chrismass wataporomosha nyimbo mpya ambazo wanarekodi katika kipindi hiki pamoja na kukumbushia nyimbo zilizotamba enzi hizo kama Fadhira kwa wazazi ya Rogath hega Katapila,Mwaka wa tabu na zinginezo


Wapenzi na mashabiki wa Bendi ya Extra Bongo wajitokeze kwa wingi kushuhudia mambo mapya ya Bendi yao na pia kukaa pamoja katika kukaribidsha kuzaliwa kwa Yesu Kristo yaani Chrismas


Bendi hiyo jumapili itaendelea na shoo katika Ukumbi wa Magereza yaani sikukuu yenyewe na juma lijalo itarejea katika ratiba yake ya kawaida.

Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza wakati wa onyesholao la katika Ukumbi wa Sun Cirro Sinza Dar es Salaam WakichezaRapa wa Bendi ya Extra Bongo, Saullo Fagason akiimba wakati wa shoo ya bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Sun Cirro Sinza Dar es SalaamRapa wa Bendi ya Extra Bongo, Saullo Fagason akicheza sambamba na wacheza shoo wa Bendi hiyo wakati wa shoo ya bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Sun Cirro Sinza Dar es Salaam Wakicheza Chocky akiimba Wacheza shoo wakichezaWacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo, Danger Boy na Husna wakicheza kwa staili ya pekee wakati wa shoo ya bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Sun Cirro Sinza Dar es Salaam

0 maoni:

Post a Comment