Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Saturday, January 14, 2012

EXTRA BONGO SASA TISHIO TANZANIA

Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza kwenye Ukumbi wa Meeda Sinza Jijini Dar es Salaam wakati wa onyesho lao la kila wiki
Wakicheza

Na Michael Macellah

BENDI ya Muziki wa Dance inayotikisa jiji la Dar es Salam na Tanzania nzima,Extra Bongo Next Level baada ya kukonga nyoyo za wapenzi na mashabiki katika kipindi cha sherehe za X-Mass na Mwaka mpya sasa wanaelekea kujikita na kurekodi nyimbo zao zilizosalia ili kukamilisha Albamu yao ambayo mpaka sasa hawajaipatia jina.


Akizungumza na mtandao huu,Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Chocky ameanza kwa kuwashukuru wapenzi na mashabiki kwanza kwa kuiunga mkono Bendi ya Extra Bongo katika kipindi chote cha siku Kuu na kuwaomba sasa wakae mkao wa kusubili mambo mapya na mazuri ya bendi hiyo ambayo watawatambulisha hivi punde mara tu ya kumaliza kurekodi.


Amesema Chocky 'tunaingia jikoni kupika vinavyopikika tunaamini tunachowaandalia mtakipenda na mtakifurahia hivyo kaeni mkao wa burudani muda si mrefu tutawafahamisha'.


Chocky amesema Bendi katika kuhakikisha inaweka mambo sawa kila mahali katika safu mbalimbali ndani ya Bendi, Bendi imeongeza waimbaji wawili,Kaba tano na Redo walikuwa TOT na wa tatu ni rapa ambaye alipumzika muda fulani lakini sasa amerejea kazini.


Katika safu ya wapiga vyombo pia ameongeza mpiga bass,tumba,drum na soro na katika safu ya wacheza shoo imeongeza watatu wa kike akiwemo Janeth Tingisha aliyekuwa Diamond Sound na mmoja wa kiume. Wacheza shoo na waimbaji wakicheza Waimbaji na wacheza shoo wakicheza kwa pamoja


0 maoni:

Post a Comment