Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Friday, March 16, 2012

FATUMA KIBORORONI APUMZIKA RASMI.

Na Michael Machellah
MCHEZA shoo marufu wa Bendi ya Extra Bongo Next Level, Fatma Kibororoni amepumzika rasmi kucheza kwenye bendi hiyo baada ya kupata ujauzito ambao umemlazimu afanye hivyo baada ya miezi kadhaa kwa sasa.

Akizungumza na mwandishi wetu Kibororoni alisema nikiendelea kung'ang'ania kucheza wapenzi na mashabiki watanishangaa kwani tumbo lake kwa sasa linaonekana kuwa ni mzamzito.

Kibororoni alisema anashukuru Uongozi wa Bendi ya Extra Bongo haswa Kiongozi wake wa upande wa shoo, Super Nyamwela kukubaliana na hali aliyonayo hivyo kumpa nafasi ya kupumzika mpaka pale atakapojifungua na atakapoona hali inamruhusu ni anaruhusiwa kurudi kazini.

Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo alisema Ujauzito kwa mtoto wa kike ni sehemu ya maisha, Fatma Kibororoni ni mwanamuziki wa Extra Bongo na ataendelea kuwa,tumempa mapumziko na tutaendelea kumwangalia na kumtunza ikiwa ni mwanamziki wetu mpaka pale atakapoona hali inamruhusu kurudi tena stejini tena.

Fatma Kibororoni alikataa kumtaja aliyempa ujauzito huo lakini akabaki kusisitiza kuwa ni mwanamziki marufu hapa nchini na muda utakapofiaka wakumtambua mtamtambua kwani kuna taratibu za mila na desturi anazikamilisha ili waweke mambo yao safi.

0 maoni:

Post a Comment