Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Tuesday, January 21, 2014

MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA MZEE MAKAMBA

 Mzee Yusufu Makamba akishauriana jambo na mwanae January Makamba wkati wa shughuli za mazishi zikiendelea. Mzee Yusufu Makamba amefiwa na mama yake mzazi aliyefahamika kama Mariam Masau Kivugo  kilichotokea tarehe 21 January 2014.
 Mzee Yusufu Makamba akiwa na mwanae January Makamba wakitafakari jambo baada ya kupata msiba mkubwa  wa kufiwa na Mama mzazi wa Mzee Yusufu Makamba, Mariam Kivugo.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Ndugu Abdallah Majura Bulembo akitoa salaam za pole kwa wafiwa wakati wa mazishi ya Bibi Mariam Masau Kivugo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa salaam za pole kwa niaba ya Chama  kwa Mzee Yusufu Makamba na Familia yake wakati wa mazishi ya Mama wa Mzee Yusufu Makamba.
 Mamia ya watu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba wakati akitoa salaama za shukrani kwa niaba ya familia kwa wananchi wote waliojitokeza kwenye mazishi ya Bibi yake Marehemu Mariam Masau Kivugo yaliofnyika Mehazangulu,Tanga.
 Mwili wa Marehemu Mariam Kivugo ukipelekwa msikitini kwa ajili ya kuombewa kabla ya kuelekea makaburini.
 Watu wakiwa kwenye nyuso za huzuni wakati wa mazishi ya Bibi Mariam Kivugo ambaye pia ni mama wa Mzee Yusufu Makamba.
 :
Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kuweka udongo kwenye kaburi la mama wa Mzee Yusuf Makamba aliyefariki tarehe 20 Januari 2014.

WAFANYAKAZI WA KAMAGA FERY WAGOMA KUSHINIKIZA BAADHI YA VIONGOZI KUTOLEWA NA HUDUMA YASIMAMA KWA MASAA KADHAA.














Na Peter Fabian.
G. Sengo blog.
MWANZA.
WATUMISHI wa Kampuni ya Kamanga Fery ya Wilayani Sengerema leo wameweka mgomo ukishinikiza kuondolewea kwa watumishi wenzao wawaili na kusimamisha utowaji huduma ya usafiri wa abiria na magari Jijini hapa.

Hatua hiyo ilielezwa na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi Adamu Yusufu ambaye pia ni Kepteni wa kivuko cha MV Orion cha Kampuni ya Kamanga Fery Ltd. kinachotoa huduma kati ya Kamanga Wilayani Sengerema na Kamanga Jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo Mwenyekiti Kapteni Yusufu alisema kwamba wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa ujumla wao wameamua kugoma kutoa huduma ili kushinikiza Mkurugenzi Wiebke Gaetye kuwaondoa watumishi Renatus Manyanda (Meneja rasilimali watu) na Anna Malapa (Mhasibu matumizi) kutokana na kuwanyanyasa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.

Mwenyekiti huyo alitaja sababu za mgomo huo kuwa ni pamoja na Manyanda kuwafukuza watumishi bila kosa, kushindwa kulipa makato ya mishahara yao kwenye Mfuko wa Jamii (NSSF), kushindwa kulipa mishahara zao kwa wakati ambapo wanadai tangu mwezi Novemba mwaka jana na kushindwa kufanya matengenezo ya vivuko vya kampuni hiyo kwa wakati.

“Bila Mkurugenzi kuyashughulikia haya tunayolalamikia ikiwa ni pamoja na kutuondolea watumishi hawa wanaolalamikiwa na wenzao, nasi hatuko tayari kufanya kazi na tutaendelea na mgomo hadi kilio chetu kitakaposikilizwa na kutolewa majibu” alisisitiza.

Kwa upande wa Mhasibu Malapa alisema kwamba amekuwa akiwanyima malipo yanayoizinishwa na Mkurugenzi ama uongozi wa Kampuni hiyo na hata amekuwa akitoa kauli za kuwakejeli watumishi wenzake jambo ambalo wamedai kuchoshwa nalo.

Kufatia mgomo huo uliodumu kwa masaa kadhaa na kupelekea Mkurugenzi Gaetye kuchukua jukumu la kukaa na wafanyakazi ili kusikiliza hoja na malalamiko yao ambapo aliamua kumfukuza kazi kwanza Manyanda kisha kusikiliza malalamiko mengine ili kupoza hasira za wafanyakazi hao.
Akizungumza madai ya wafanyakazi hao Mkurugenzi huyo alisema kwamba tayari amemfukuza kazi huku hoja za malipo ya mishahara yao ataifanyia kazi haraka na ile ya NSSF huku Mhasibu Malapa akisimamishwa kwanza kuchunguzwa na uamuzi wake ukisubili kikao cha uongozi wa Kampuni.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi (Cotwu) tawi la Kampuni hiyo Kapteni Jorwa Magesa (MV Orion) alisema kwamba kufatia kikao na Mkurugenzi wao wamelidhika na hatua alizochukua na wamempatia muda kushughulikia mambo mengine yaliyosalia ikiwa ni malalamiko yao ya msingi.

Hatua ya kuondolewa kwa Manyanda imepongezwa na wafanyakazi na wananchi wa Kijiji cha Kamanga Wilayani Sengerema ambao juzi majira ya jioni waliandamana na mabango kumpinga kuendelea kuwa mfanyakazi wa Kampuni hiyo hali hiyo ilipelekea jana kuwepo mgomo mkali kwa wafanyakazi hao nao wakipinga kuendelea kuwepo kwa watu hao katika Kampuni hiyo.

Manyanda pia amelalamikiwa na baadhi ya wafanyakazi waliokataa kutajwa majina yao hadharani kwa madai kuwa Manyanda alikuwa akitumia pia Jina la Mama Salma Kikwete kumtishia Mkurugenzi huyo raia wa Taifa moja la Ulaya kuwa akimfukuza naye ataondolewa nchini.

Hadi tunakwenda mitamboni hali ya eneo la Kamanga fery ilikuwa shwari baada ya Mkurugenzi na wafanyakazi wake kukubaliana kuendelee kutolewa huduma ya usafiri wa abiria na magari wakati madai yao mengine yakishughulikiwa na kuchukuliwa hatua za haraka kama walivyokubaliana.

MVUA YATISHIA AMANI MWANZA NA KANDA YA ZIWA KWA UJUMLA


Barabara ya Lumumba jijini Mwanza na heka heka zake katika kipindi cha mvua.
Mifereji ya maji taka ni finyu nayo ikishinda bila kufanyiwa usafi ikiwa ni pamoja na uzibuaji hali huwa tete.
Adha waipatayo wafanyabiashara waliopangisha kwenye maduka ya majengo yaliyopo pembezoni kwa kituo cha daladala za Mwaloni zamani karibu na soko kuu.
Mitaro imejaa, barabara zimejaa maji, Si biashara tena bali sasa ni kila mmoja kuokoa mali zake.
Chepe chepe...dugu yake tepe tepe.
Ili kuepuka kadhia hii ambayo kama mvua ingenyesha nyakati za usiku ingekuwa hasara kubwa kwa mali zilizowekwa sakafuni, basi ni jukumu sasa la kila mfanyabiashara kuhakikisha takataka za maboski, mifuko, vitambaa na bidhaa nyingine za kutupa, kuwa zinahifadhiwa kwenye mapipa maalum ya taka na si kuyaelekeza kwenye mifereji ya maji taka.

ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE APEWA MISAADA.









WADAU mbali mbali na wasamaria wema wamezidi kujitokeza kumpa msaada wa hali na Mali,Aida Nakawala(25) mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, aliyejifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadruplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya.
Misaada hiyo imeongozana ikiwa ni siku moja baada ya Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Vanesa pamoja na Mbeya yetu kutoa misaada mbali mbali ambapo leo Kampuni ya Arif Electronic nayo imeguswa.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo pamoja na familia yake, Faizar Kasamia, baada ya kuguswa na hali ya Mama huyo ametoa vitu vya aina mbali mbali vyenye thamani ya Shilingi Laki tatu.
Vitu alivyotoa ni pamoja na Nguo,Maziwa (Lactogen), Mafuta, Sabuni na Nepi.

0 maoni:

Post a Comment