Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Wednesday, April 23, 2014

SAFARI LAGER YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA VYUO VINAVYOSHIRIKI FAINALI ZA HIGHER LEARNING POOL COMPETITION 2014 JIJINI DAR ES SALAAM.


 
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu(wa pili kulia) akimkabidhi t-shirt nahodha wa timu ya mabingwa watetezi wa mashindano ya Safari Pool ya Elimu ya juu, Abubakar Amri wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo vya Dar es Salaam vinavyoshiriki fainali za Safari Higher Learning Pool Competition 2014.Makabidhiano hayo yalifanyika Coco Beach Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo na Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
 
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu(wa pili kulia) akimkabidhi t-shirt mwakilishi wa chuo cha DSJ, Mwajuma Kitwana wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo vya Dar es Salaam vinavyoshiriki fainali za mkoa  za Safari Higher Learning Pool Competition 2014.Makabidhiano hayo yalifanyika Coco Beach Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo na Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
 
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu(wa pili kulia) akimkabidhi t-shirt mwakilishi wa chuo cha Mwl.Nyerere, Nelson Fred wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo vya Dar es Salaam vinavyoshiriki fainali za mkoa  za Safari Higher Learning Pool Competition 2014.Makabidhiano hayo yalifanyika Coco Beach Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo na Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga. 
 
Meneja wa Bia ya Safari Lager,  Oscar Shelukindo(kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo vya elimu ya juu iliyofanyika Coco Beach Dar es Salaam.Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu na Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.
 
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu(wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo vya elimu ya juu iliyofanyika Coco Beach Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.

 
Meneja wa Bia ya Safari Lager,  Oscar Shelukindo(kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi vifaa vya michezo kwa vyuo vya elimu ya juu iliyofanyika Coco Beach Dar es Salaam.Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu na Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.


 Kampuni ya Bia nchini Tanzania (TBL) leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa Vyuo vya elimu ya juu vitakavyoshiriki fainali za mashindano ya Pool yajulikanayo kwa “Safari Higher Learning Pool Competition 2014
Mashindano haya yalianza Tarehe 12 Aprili 2014, yakishirikisha mikoa minane nchini, ambapo yalianzia Iringa,Mbeya,Morogoro,Kilimanjaro,Dodoma na Arusha kwa ngazi ya mikoa.
Wiki hii fainali hizo zitahitimishwa kwa mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza kwa ngazi ya mikoa.
Dar es Salaam vyuo vilivyothibitisha kushiriki ni Chuo cha Mwalimu Nyerere, UDSM, DUCE, MSJ, RCT, TSJ, ST.JOHN, Intitute of Social Work, DIT, TIA, OPEN UNIVERSITY, ARDHI,DSJ, IFM na mabingwa watetezi CBE.
Faianali za Dar es Salaam zitafanyika 26 na 27 April 2014,katika viwanja vya Coco Beach zikisindikizwa na Burudani ya Msanii wa muziki wa nyimbo za kizazi kipya Joel Makini(Mwamba wa Kaskazini).
Mwanza vyuo vilivyothibitisha kushiriki ni Chuo cha Bugando, TIA, CBE na mabingwa watetezi St.Augustine.

Fainali za Mwanza zitafanyika 26 April 2014 katika Ukumbi wa Shooters Club ambapo pia msanii wa muziki wa nyimbo za kizazi kipya Joel Makini(Mwamba wa kaskazini).

 Fainali za kitaifa zinatarajiwa kufanyika Juni 3 na 4,2014 mkoani Kilimanjaro. Ni mwaka wa tano sasa mashindano haya yamekuwa yakiendelea na kwa miaka yote shindano hili limekuwa moja kati ya michezo mikubwa kwenye calendar ya mwaka ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya Juu.

“Imebainika duniani kote kwamba michezo inanguvu ya kuwaleta watu pamoja, kufundisha na kukuza vipaji na vile vile kujenga afya bora. Tunajivunia kwa mara nyingine kuwa wadhamini wa mchezo huu, ambapo wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali watakutana na kushindana kwenye mazingira mazuri”, alisema Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo said.

0 maoni:

Post a Comment