Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Friday, July 11, 2014

BancABC WAFUTURISHA WATEJA WAO PAMOJA NA WAFANYAKAZI SERENA HOTELI JIJINI DAR ES SALAAM.


 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum(kulia) akizungumza na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakati futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.Kushoto niMkuu wa Huduma za kifedha wa BancABC,  Mwalimu Zubery. 


 Na Mwandishi Wetu
SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum amewaomba waamini wa dini ya Kiislamu kusameheana katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwasaidia wanaohitaji msaada.

Sheikh Alhad aliyasema haya wakati wa futari iliyoandaliwa na BancABC jana katika Hotel ya Serena kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo.

"Kwa niaba ya jamii ya Waislamu ningependa kuwashukuru BancABC kwa kuandaa futari jioni ya leo ili kukumbushana katika Imani yetu ya dini ya Kiislamu. Napenda kuwaomba ndugu na jamaa wote kukaa karibu na Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki, tukumbuke  kusameheana, kuwasaidia wale wanaohitaji msaada na kusimama imara Imani. Pia, naipongeza BancABC kwa kutambua mahitaji ya jamii yetu hasa wafanyakazi wa serikalini na kuamua kuanzisha bidhaa mpya ya Mkopo Rahisi iliyoenea nchi nzima. Nawatakia kila la kheri katika kutimiza majukumu yenu ya kila siku ili kuwapatia wateja wenu huduma bora zenye kiwango cha kimataifa.”, alisema Sheikh Al-haad Mussa.

Nae Mkuu wa Huduma za kifedha wa BancABC,  Mwalimu Zubery alisema, "BancABC inawathamini sana wateja wake na ni heshima sana kwetu kujumuika na ndugu zetu kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tungependa kuwashukuru wateja wetu kwa ushirikiano wenu, hafla kama hizi zinatusaidia kuwafahamu wateja wetu vizuri ili kuweza kuwapa Huduma bora zaidi”.

Mwalim Zubery alimalizia kwa kusema, "Tungependa kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuchagua BancABC na tunapenda kuwakumbusha wateja wetu ambao wataenda Kuhijji Macca baadaye mwaka huu watembelee matawi yetu na kupata kadi ya VISA kwa ajili ya kusafiri. Kadi hiyo ya VISA inahakikisha urahisi na usalama wa pesa zako uwapo popote duniani. Wateja wana fursa ya kuchagua kati ya kadi mbili za VISA za malipo ya kabla, moja ikiwa ni Cash Card na nyingine ni Travel Money Card. Kadi hizi ni salama kwa kuhifadhi fedha zako uwapo safarini nje na ndani ya nchi." 
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum(kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakimsikiliza mgeni rasmi, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum(hayupo pichani) wakati wa futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa wakichukua futari iliyoandaliwa na BancABC kwa wateja na wafanyakazi wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jana. 

WADAU WA BIA YA NDOVU SPECIAL MALT WAFANYA BONGE LA PARTY JIJINI MBEYA BAADA YA BIA HIYO KUTWAA TUZO YA UBORA WA KIMATAIFA.

 Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli(wa pili kulia), akigonanija chupa za bia ya Ndovu Special Malt  na wadau wa bia hiyo wakati wa  hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mbeya hivi karibuni.
 Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akizungumza na wadau wa bia hiyo wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.
 Wadau wakipata Bia ya Ndovu Special Malt wakati wa  hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.

MTAMBO WA GONGO KUZICHAPA NA MUDI MBABE JUMAPILI YA AGOSTI 10,2014 CCM MWINJUMA MWANANYAMALA.

 Promotor wa mbambano wa ngumi za usiokuwa na ubingwa, Rashid Kipanga akiwatambulisha, Manenono Osward(Mtambo wa Gongo) kulia na Abdalah Pazi(Mudi Mbabe) wanaotarajia kuchuana Augosti 10,2014.Makubaliano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Mwinjuma Dar es Salaam. 
 Na Mwandioshi Wetu.
BONDIA Mkongwe wa masumbwi, Maneno Osward maarufu kwa jina la “Mtambo wa gongo” jana amesaini rasmi kuzichapa na bondia chipukizi Mohamed Pazi maarufu kwa jina la “Mudi Mbabe”.
Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) alisaini jana huku akimtahadhalisha mpinzani wake kuwa yeye hachagui umri,bali mtu yeyeto ambaye yuko tayari na vigezo vimezingatiwa vya Chama cha Ngumi nchini yeye yuko tayari muda wote.
Mtambo wa gongo wa Gongo alitamba kuwa kijana bondia chipukizi anayejiita Mudi Mbabe anataka kumbadilisha jina na kuwa Mudi mnyonge  na katika raundi 6 zilizopangwa hatafika mwisho.
Nae Abdalah Pazi bondia chipukizi alitamba yeye hataki ngojela atakachokifanya kwa anayejiita mkongwe wa masumbwi kitakuwa historia katika maisha yake kwani hatafika raundi ya nne.
Mwisho Mudi aliwataka wapenzi na mashabiki wa Ngumi kujitokeza kwa wingi hususani madereva bodaboda ambao ndio wafanyakazi wenzake wajitokeze kwa wingi kumshangilia atakavyomfanya vibaya Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) na kumbadilisha jina kuwa Mtungi wa maji.
Mbambano wa Maneno Osward(Mtambo wa Gongo) na Abdalah Pazi(Mudi Mbabe) umedhibitishwa na Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TBBC), Chaurembo Palasa ambaye aliwataka mabondia wasiwe chanzo cha fujo katika mpambano huo ikiwa ni kukuza na kuendeleza mchezo wa Ngumi nchini.
Mpambano huo utakuwa ni wa KG 78-Super middle weight utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam tarehe Augosti 10,2014 kuanzia saa kumi na mbili.
Wasanii watakaotoa burudani katika mbambano huo ni Kikosi cha Mizinga chini ya Uongozi wa Karapina,Sster P pamoja na wengine wengi.
Mgeni rasmi katika mbambano  huo ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge.
 Mchezaji wa Nngumi, Maneno Osward(Mtambo wa Gongo) akisaini mkataba wa kupigana na Abadalah Pazi(Mudi Mbabe) Augosti 10,2014 katika Ukumi wa CCM Mwinjuma jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TPBC), Chaurembo Palasa akishuhudia
Mchezaji wa Nngumi, Abdalah Pazi(Mudi Mbabe) akisaini mkataba wa kupigana na Abadalah Pazi(Mudi Mbabe) Augosti 10,2014 katika Ukumi wa CCM Mwinjuma jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TPBC), Chaurembo Palasa akishuhudia. 

0 maoni:

Post a Comment