Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Monday, September 22, 2014

RAIS KIKWETE AHUDHURIA HAFLA YA KUMPONGEZA KWA UONGOZI MZURI YA USIKU WA KAKAYA.

Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane aliejitambulisha kwa jina la Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Dkt Seche Malecela baada ya kupokea risala ya pongezi kwa uongozi wake nchini Tanzania  katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea makombe toka kwa Balozi wa Heshima wa Tanzania huko California Mhe Ahmed Issa kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka Watanzania kutoka Atlanta  kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka Watanzania kutoka Atlanta  kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete akiwa na mtoto wa miaka minane Brian ambaye alitoa burudani ya kupiga kinanda wakati wa wimbo wa Taifa na nyimbo nyinginezo katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokea zawadi ya ngao na kikombe toka kwa  mwakilishi wa  CCM New York na Vitongoji vyake  Bw. Isaack Kibodya  kama pongezi kwa uongozi uliotukuka Rais Jakaya Kikwete katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington. Kombe hilo ni la pongezi kwa ulezi wake katika michezo na sanaa nchini Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika hafla ya USIKU WA JAKAYA uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya JW Mariott jijini Washington.
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi.

AMPUNI YA VIFAA VYA KIELEKTRONIKI SAMSUNG YALENGA KUKUZA UCHUMI WA JIJI LA ARUSHA.




Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Samsung inazindua rasmi duka kubwa na kituo chake cha huduma kwa wateja lililopo barabara ya Sokoine mjini Arusha siku ya leo. Uzinduzi huo utawawezesha wateja wake wote mkoani Arusha kupata huduma stahiki na bidhaa halisi za Samsung. Kituo hiki ni cha kwanza kuzinduliwa mkoani Arusha na kampuni kubwa ya kimataifa ya kielektroniki.
“Mtazamo wa maisha ya wateja hubadilika kwa kasi kubwa na kuwafanya kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma bora. Kama kampuni kubwa inayoongoza kuwa na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni, Samsung imefanya juhudi kubwa kuhakikisha inatimiza mahitaji ya wateja wake wote Afrika. Mkoa wa Arusha hutegemea sana biashara kwani una wakaazi toka jamii mchanganyiko. Hivyo katika Afrika Mashariki, Arusha ni kitovu cha wageni toka nchi mbalimbali ulimwenguni. Kampuni ya Samsung ina imani kubwa kwamba kituo cha huduma kwa wateja kitatoa ushirikiano mzuri na kuboresha uhusiano kwa wateja wake mkoani Arusha. Kwasababu Arusha ni kituo kikuu cha safari nchini Tanzania”, haya yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa kampuni hii nchini Tanzania, Bw. Seo
Kituo hiki kitatoa huduma za ziada kwa wateja wa Samsung mbali na kuuza simu za mkononi na bidhaa za kielektroniki. Hii ni pamoja na kuwapa wateja wake watakaojisajili na huduma ya e-warranty (dhamana) usaidizi wa kiufundi bila malipo kwa kipindi cha miaka miwili.
Mpango huu utawanufaisha wateja wa Samsung watakaosajili bidhaa zao kupitia Simu. Huu ni mchakato utakaofanyika kwa kutuma namba ya IMEI kwenda 15685. Baada ya kufanya hivyo wateja watanufaika na msaada wa kifundi kwa kipindi cha miaka miwili sambamba na kujipatia nafasi ya kushinda bidhaa mbalimbali za Samsung.
Katika kusherehekea uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinawasogezea wateja wake huduma karibu, kampuni hii kubwa duniani inawaletea habari njema wakaazi wa Arusha kwa kutoa punguzo kubwa la bei za bidhaa zake. Kwenye kipindi hiki cha ufunguzi bidhaa zitakazokuwa na punguzo la bei ni pamoja na; Luninga, feni, majokofu na vifaa vya nyumbani. Bila kuwasahau wateja wake wa simu, vifurushi vya intaneti na zawadi za T-shirts zitatolewa kwaajili ya wanunuzi wa simu aina ya Galaxy Trend lite.
Kwa sasa nchini Tanzania kampuni ya Samsung ina maduka na vituo vya huduma kwa wateja katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam na ina mipango kabambe kuongeza huduma zake mikoa mingine.
Duka hili na kituo chake cha huduma kwa wateja vitatoa huduma siku za wiki yaani Jumatatu-Ijumaa kuanzia saa 9.30 asubuhi hadi 5.00jioni kwa Jumamosi ni kuanzia saa 9.30asubuhi hadi 1.00 mchana, litafungwa siku za Jumapili na Siku kuu.

0 maoni:

Post a Comment