Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Thursday, October 30, 2014

SAFARI LAGER YAZINDUA RASMI PROGAMU YAKE YA “SAFARI LAGER WEZESHWA” KWA MSIMU IV, 2014.

 Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kushoto) akiwaonyesha kipeperushi cha shilingi 2200,000 000/= zitakazogawiwa kwa wajasiliamali wakati wa uzinduzi wa prpgramu ya Safari Wezeshwa msimu wan ne uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jaji wa programu hiyo, Joseph Mmigunda.
  KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imeziduwa rasmi programu yake ya Safari  Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa wajasiriamali wadogo wadogo Nchini.  

Akizungumza  na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo  alifafanuwa ya kwamba “ programu hii ni hazina tosha kwa wajasiriamali wadogowadogo nchini kwani itarahisisha kazi  kwa kuwepo na vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi”.

Programu hii ni msimu wa nne tangu kuanzishwa kwake na  imeleta mafanikio makubwa kwa wajasiriamali waliopata uthubutu wa kujaribu kujiunga na hatimae kuongeza uchumi wa nchi.

Bw. Oscar alifafanuwa kuwa, Programu hii itafanyika takribani mikoa yote Nchini ambapo fomu zitaanza kutolewa kuanzia leo kupitia mtandao wa www.wezeshwa.co.tz na baadae kusambazwa katika mabohari na viwanda vya TBL nchi nzima.Hii itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia kujaza fomu kwa usahihi na kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae waliokidhi nafasi zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi  pamoja na kukabidhiwa ruzuku  zao. 

Nae Jaji kutoka TABDS, Bwana Joseph Migunda alisema kuwa  “Zoezi hili linahusisha majaji wenye utaalamu na  wenye umakini  kwa namna moja au nyingine.Hivyo aliomba wajasiriamali wote wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye  malengo ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hii”.
Jaji wa programu Safari Wezeshwa kutoka Kampuni ya TABDS, Joseph Mmigunda(kulia)  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa program hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

RAIS KIKWETE AWASILI VIETNAM KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI.

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mhe Truong
Tan Sang wakikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake
wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya
kwanza ya ziara yake rasmi  ya siku mbili nchini humo leo Jumatatu
Oktoba 27, 2014
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua akishuhudiwa
na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam  wakati wa
mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya
ziara yake rasmi  ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa  na mwenyeji wake Rais Mhe
Truong Tan Sang wa Vietnam  wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu
ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi  ya siku mbili
nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu
Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong,
katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo
Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana baada ya
kutembelea kampuni ya mawasiliano ya VIETTEL Jumatatu Oktoba 27, 2014

0 maoni:

Post a Comment