Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Monday, January 25, 2016

KIKUNDI CHA HAPA KAZI –UKEREWE MABINGWA MBIO ZA MAKASIA 2016.



Mabingwa wa mbio za Balimi Boat Race 2016 wakishangilia mara baada ya kushinda mbio za kupiga makasia wakitumia dakika 34. Mashindano mbio za Makasia ni mara ya 16 yakidhaminiwa na TBL kupitia bia ya Balimi Extra Lager,ambayo yalishirikisha vikundi 15 vya mkoa wa kimechezo wa Ukerewe
Na Mwandishi wetu,UKEREWE
VIKUNDI vya Wazee wa Mamba (Wanauame)na Hapa Kati tu  ( Wanawake),vya mkoa wa Michezo wa Ukerewe, vimevunja rekodi ya mashindano ya mbio za Mitumbwi za Balimi Boat Race 2016 na kutwaa ubingwa na kujinyakulia vikombe medali za dhahabu na fedha taslimu sh.2.2.
 
Mashindano hayo yalifanyika juzi kwenye ufukwe wa Monarch hoteli wilayani Ukerewe, ambapo mgeni rasmi Mkuu wa wilaya hiyo, Josephat Mkirikiti alikabidhi zawadi kwa washindi wa mivhuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia ya Balimi Extra Lager.
 Bingwa wa mashindano hayo kwa upande wa wanaume, kikundi cha Wazee wa Mamba kilitumia dakika 31 kuweza kutwaa ubingwa huo na kukabidhiwa kombe,medali za dhahabu na fedha taslimu, sh.1.2 ,huku Kikundi cha Hapa Kazi tu kwa wanawake,kiling’ara kwa kushika nafasi ya kwanza, kikitumia dakika 39 na kukabidhiwa fedha taslimu sh. 1,000,000,medali za dhahabu na kombe. 
Nafasi ya pili kwa wapiga makasia hao kwa wanaume ilikwenda kwa kikundi cha Kama Ipo Ipo tu kwa kutumia dakika 34 na kujinyakulia kitita cha sh.1,000,000, kikundi cha Ya Mtoto  kilinyakua nafasi ya tatu baada ya kutumia dakika 35 na kulamb sh.800,000 na  nafasi ya nne ilinyakuliwa na kikundi cha Tuliochelewa ambacho kiliondoka na sh.600,000.
Vikundi vya Usipoteze muda, Nani Kaona,Maisha ni kutafuta ,Mbeya City, Hapa Kazi tu na Ole wenu,vilivyoshika nafasi ya tano hadi ya kumi,kila kimoja kilipata kifuta jasho cha sh.250,000.
Kwa upande wa wanawake,nafasi ya pili ilikwenda kwa kikundi Kaza Roho,ambacho kilitumia dakika 41 na kikapata sh.800,000, kikundi cha  tatu cha Kazi na Malengo, kilitumiaz dakika 43 na kubeba sh.600,000 na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Upendo na kuzawadiwa sh.400,000.
Hata hivyo katika mashindano hayo kikundi cha nahodha Yasinta kutoka Kirumba mtumbwi wazo ulipinduka na kuzama lakini baada ya kuokolewa walibadili mtumbwi na kuendelea mashindano na ukashika nafasi ya tisa.
Vikundi vitatu vy tabia Njema, Mtafuta cha Uvunguni na Eberneza vilivyoshika nafasi ya tano hadi ya saba walifutwa jasho kwa sh.200,000 kila kimoja, hata hivyo vikundi vitatu viliondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kubainika vilishiri mashindano kama hayo kwenye mikoa ya Mara na Mwanza, kimoja kikikishika nafasi ya kwanza na kingine nafasi ya pili.
Akizungumza wakati akikabidhi zawadi, Mkuu wa Wilaya, Mkirikiti, alisema kampuni ya TBL isichoke kupeleka mashindano kama hayo wilayani humo kwa sababu wananchi wake wanapenda michezo na burudani.
“TBL niwapongeze mnafanya vizuri katika eneo la kodi,mmekuwa marafiki wa Uerewe sababu mmetufanya tuwe sehemu ya maisha yenu.Changamoto yenu mtuangalie katika sekta za afya na elimu (madawati).Mtusaidie hili la madawati na tupo tayari kuondoa vikwazo vinavyowakwaza  ili tuondokane na kero ya madawati,”alisema Mkirikiti.
Pia, aliipongeza kampuni hiyo kwa kuwaondoa washiriki (mamluki) waliokwisha shiriki mashindano hayo mikoa mingine,ambo walikuja kuchukua nafasi zizizo za kwao na katika eneo lisilo la kwao.
Aidha, Meneja Mauzo wa TBL Kanda ya Ziwa, Godwin Zacharia,alisema lengo la TBL kwa miaka 16 ya mashindano ya Balimi, ni kukuza utamaduni na michezo ukiwemo wa kupiga makasia .
Alisema, kutokana na kukubaliwa na jamii ya Kanda ya Ziwa,wataendelea kuyaboresha kwa kuongeza zawadi na washiri kila mwaka kwa sababu bado wana kiu na kuahidi kushughulikia changamoto ya washiriki bandia . 
                             
Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Mitumbwi Taifa-Tanzania Canoe Assocition,(TCA) Richard Mgabo alisema kuwa, akiwa mwasisi wa mashindano ya makasia,anafarijika kuona mchezo huo ambao haukuwepo nchini, ukipata mashabiki na kuzidi kupendwa na wananchi wa kada mbalimbali na kuishukuru TBL kwa udhamini wao tangu yaanzishwe.
 Mashindano hayo Balimi Boat Race  yamefikisha umri wa miaka 16 tangu yaanzishwe mwaka 2000, kwa udhamini wa TBL kupitia kinywaji chake cha bia ya Balimi Extra Lager,ambapo mwaka huu Ukerewe yamefanyika kwa hadhi ya kimkoa baada ya wilaya hiyo kupewa hadhi ya mkoa.Fainali ya mwisho itafanyika Januari 30, mkoani Geita.

2 maoni:

Bongo Exclusive said...

Hellow Nice Blog! Visit https://www.bongoexclusive.net

John said...

Basics for Beginners in Online Trading

Post a Comment