Subscribe:

Ads 468x60px

Pages

Friday, August 16, 2013

RATIBA YA FAINALI ZA MASHINDANO YA TAIIFA YA MCHEZO WA POOL NGAZI YA MIKOA KUANZA WIKI IJAYO AGOSTI 23,2013 “SAFARI LAGER NATIONAL POOL CHAMPIONSHIPS 2013”.

 Katibu wa Chama cha Pool Taifa(TAPA),Amos Kawinga(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu muendelezo wa ratiba ya mashindano ya Safari Pool Competitions 2013 jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanziania(TBL), Fimbo Butallah
Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Butallah akizungumza
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Pool Taifa(TAPA) leo kimetangaza ratiba ya muendelezo wa mashindano ya mchezo wa Pool Taifa ngazi ya mikoa unaotarajiwa kuendelea Agosti 23,2013 katika mikoa iliyobaki yajulikanayo yajulikanayo kama “Safari Lager National Pool Championships 2013” yanafanyika kwa mwaka wa sita sasa, Safari Lager imekuwa wadhamini wakuu wa mashindano haya kwa miaka yotesita.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam  Katibu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga alisema baada ya mapumziko ya mfungo wa Ramadhani sasa ratiba ya Fainali za mashindano ngazi ya mikoa tutaendelea na mkoa wa Dar es Salaam ambao unamikoa mitatu ya kimichezo ambapo 23 Agosti,2013 mikoa yote itaanza fainali zake na Agosti 25,2013 wataanza mkoa wa Temeke kumaliza wakifuatiwa na mkoa wa Ilala Agosti,311,2013 na mwisho watamalizia Mkoa wa Kinondoni Sepemba 01,2013.
Katibu alisema fainali za mwaka zilianza juni 27,2013 kwa kushirikisha mikoa 17 na tayari baadhi mikoa imeshamaliza na kupata klabu itayowakilisha mkoa katika mashndano ya kitaifa Mkoani Morogoro Septemba 08,2013 kama linavyonyesha jedwali hapo chini;  
                      MKOA
                  KLABU BINGWA
MKOA WA LINDI
KLABU YA BUS STAND
MKOA WA KAGERA
KLABU YA BALELE
MKOA WA TABORA
KLABU YA LORIONDO
MKOA WA MWANZA
KLABU YA PASEANSI
MKOA WA SHINYANGA
KLABU YA KING PALACE
MKOA WA MOROGORO
KLABU YA ANATORY
MKOA WA ARUSHA
KLABU YA NGARENARO
MKOA WA KILIMANJARO
KLABU YA MBOSHO
MKOA WA TANGA
KLABU YA SPIDER
MKOA WA MANYARA
KLABU YA SUPERSPORT
MKOA WA PWANI
KLABU YA YAKWETU
TEMEKE-DSM
BADO
ILALA     -DSM
BADO
KINONDONI-DSM
BADO
DODOMA
BADO
IRINGA
BADO
MBEYA
BADO
Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), Fimbo Butallah alisema wao wamejipanga vizuri hasa kwenye swala la zawadi kuanzia ngazi ya Mmkoa hadi Taifa wako vizuri.
Alisema Butallah, “Nia hasa ya kudhamini mashindano haya ni kuibua vipaji kwa vijana na kuwasaidia kiuchumi hasa ukizingatia kwamba kwa sasa michezo ni ajira kama ajira nyinginezo. Mchezo wa pool huandamana pia naburudani waipatayo wachezaji kutokana na mchezo huo”. Bw. Butallah  aliendelea kusema; “Ukiachilia mbali ongezeko la kipato na burudani, mchezo wa pool husaidia kuwakutanisha watu mbalimbali kufahamiana kibinafsi na kibiashara, hujenga afya bora na katika mazingira yetu ya sasa michezo inamsaidia mtu kutumia muda wake vizuri ili kuepuka mambo mengine yanayoweza kumsababishia matatizo kama vile kukaa vijiweni, ugomvi nk”. Safari Lager imekuwa wadhamini wa mchezo wa Pool toka mwaka 2008, imedhamini mashindano ya ndani na ya nje ya nchi pia. Imedhamini timu ya Taifa ya mchezo wa Pool kushiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa Pool nchini Ufaransa mwezi wa kumi mwaka 2010 ambapo timu yetu ilifanya vizuri.

0 maoni:

Post a Comment